Mataifa mbalimbali yatakuwa viwanja tofauti vya kucheza mechi zao za pili za kuwania kushirki Kombe la Dunia 2026.
Michuano hiyo ya kufuzu kwa timu za Afrika ilianza Jumatano Novemba 15 huku timu zikisajili matokeo ya kufurahisha au kuvunja matumaini katika safari zao za kujinyakulia tiketi ya mashindano hayo.
Mechi hizo zitaendelea tena Jumatatu hii huku mechi tofauti zikiwa zimeratibiwa katika kipindi hiki cha mapumziko haya ya kimataifa.
Ratiba kamili ya Mechi za Jumatatu tarehe 20 Novemba
- Djibouti v Guinea Bissau (Kundi A) | 1500 | Cairo, Egypt
- Liberia v Equatorial Guinea (Kundi H) | 1600 | Paynesville, Liberia
- Seychelles v Kenya (Kundi F) | 1900 | Abidjan, Côte d'Ivoire
- The Gambia v Côte d'Ivoire (Kundi F) | 1900 | Dar Es Salaam, Tanzania
- Mali v Central African Republic (Kundi I) | 1900 | Bamako, Mali
- Chad v Madagascar (Kundi I) | 2000 | Oujda, Morocco
Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumapili, tarehe 19 Novemba
- Zimbabwe 1-1 Nigeria (Kundi C)
- Mozambique 0-2 Algeria (Kundi G)
- Burundi 1-2 Gabon (Kundi F)
- Sierra Leone 0-2 Egypt (Kundi A)
- Sudan 1-0 Congo DR (Kundi B)
Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumamosi tarehe 18 Novemba
- Afrika Kusini 2-1 Benin (Kundi C)
- Niger 0-1 Tanzania (Kundi E)
- Senegal 4-0 South Sudan (Kundi B)
Mechi za wiki hii ndizo za mwisho kwa timu hizo mwaka huu, kwani zitacheza mechi zao za tatu za kufuzu mwaka ujao, kati ya tarehe 3 na 11 Juni 2024.
Mshindi wa kwanza katika kila kundi kwenye makundi hayo tisa, atafuzu moja kwa moja kushiriki Kombe la Dunia
Raundi ya pili itazileta pamoja timu nne bora katika mbili moja-off nusu fainali, ikifuatiwa na fainali.
Kwa mara kwanza, kombe hilo la dunia 2026, ambalo safari hii litaandaliwa Marekani, Canada na Mexico, litakuwa na timu 48.