Kulingana na ripoti hiyo, Afrika Kusini, Misri, Nigeria, Kenya, na Morocco ndio mataifa yanayoongoza kwa matajiri wengi barani Afrika huku kwa pamoja yakichangia asilimia 56 ya watu wenye thamani kubwa ya mali na zaidi ya 90% ya mabilionea wa bara hilo.
Afrika kusini ndio taifa lenye matajiri wengi Afrika huku miji minne kati ya miji 10 ya utajiri zaidi barani Afrika ikipatikana Afrika Kusini. Jiji la Johannesburg ndilo jiji lenye mamilionea wengi Barani Afrika ikiwa na mamilionea 14,600.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni za New World Wealth, kuna takriban nyumba za kifahari 3,700 nchini Afrika Kusini ambazo zina thamani ya zaidi ya dola milioni 1. Kutokana na hili, Afrika Kusini ni mojawapo ya masoko 20 makubwa ya makazi duniani, mbele ya nchi nyingine za Afrika na kulingana na masoko makubwa yanayoibuka kama vile India na Brazil.
Orodha hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya 'Utajiri wa Afrika 2023', iliyotolewa na Henley & Partners ikishirikiana na New World Wealth.
Kulingana na ripoti hiyo, Afrika Kusini, Misri, Nigeria, Kenya, na Morocco ndio mataifa yanayoongoza kwa matajiri wengi barani Afrika huku kwa pamoja yakichangia asilimia 56 ya watu wenye thamani kubwa ya mali na zaidi ya 90% ya mabilionea wake.
Nchi ya Misri, ndio yenye idadi ya pili ya mamilionea wengi barani Afrika.
Misri ndio imetambulika kuwa nchi yenye mabilionea wengi barani Afrika huku mji mkuu wake wa Cairo, ikiwa jiji la pili lenye matajiri wafikao 7,400.
Jiji la nne lenye matajiri wa juu ni Lagos, Nigeria ikiwa na mamilionea 5,400.
Kenya ndio nchi ya nne yenye matajiri ikiwa na mamilionea wafikao 7,700.
Durban, katika nafasi ya 6 na 3,600 Na Pretoria katika nafasi ya 8 na mamilionea 2,400.
Mauritius ndio nchi ya sita yenye utajiri Afrika nyuma ya Morocco ikiwa nchi inayoorodheshwa katika nafasi ya sita.
Algeria, taifa linalofahamika kwa mastaa wa soka maarufu Afrika Kaskazini, ndio nchi inayoorodheshwa nafasi ya saba.
Ethiopia ambayo ni nchi maarufu kwa wanariadha bora Afrika, inaorodheshwa nafasi ya nane.
- Ghana ndio nchi inayoshikilia nafasi ya tisa.
- Tanzania ndio nchi inayokamilisha orodha ya nchi kumi bora.
Idadi ya mamilionea barani Afrika inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 42% katika kipindi cha miaka 10 ijayo, na kufikia karibu 195,000 ifikapo 2032, kulingana na ripoti hiyo.
Nchi hizo 10 ni kama ifuatavyo:
- Afrika Kusini
- Misri
- Nigeria
- Kenya
- Morocco
- Mauritius
- Algeria
- Ethiopia
- Ghana
- Tanzania