Mkenya Kelvin Kiptum afuzu 5 bora, tuzo ya wanariadha bora wa kiume duniani 2023

Mkenya Kelvin Kiptum afuzu 5 bora, tuzo ya wanariadha bora wa kiume duniani 2023

Wanariadha bora wa mwaka Duniani watatangazwa mnamo tarehe 11 Desemba kama sehemu ya Tuzo za wanariadha Duniani 2023
Mwanariadha wa mbio za marathon kutoka kenya, Kelvin Kiptum asherehekea ushindi wakewa mbio za Chicago, mwezi Oktoba. Picha: Getty

Baraza la Riadha Duniani na familia nzima ya riadha duniani zilipiga kura zao kwa barua pepe, huku mashabiki wakiandika maamuzi yao kutumia mitandao, kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii ya Shirikisho la Riadha Duniani ambapo jumla ya kura milioni 2 zilipigwa.

Kwa mujibu wa majina ya wanariadha watano zilizotolewa, ambao watawania tuzo za Riadha za Dunia 2023, Kelvin Kiptum ameorodheshwa miongoni mwa nyota watakaogombea taji la mwanariadha bora duniani kwa upande wa wanaume.

Kiptum alikuwa mwanariadha wa kwanza kuvunja rekodi ya saa 2: 01 kwenye mbio za Benk ya Marekani mjini Chicago tarehe 8 Oktoba, mwaka huu.

Nyota huyo alimaliza kwa muda wa saa 2:00: 35 ikiwa ni sekunde 34 chini ya rekodi ya dunia ambayo ilikuwa imewekwa na mwenzake Eliud Kipchoge huko Berlin mwaka 2022.

Licha ya kushiriki marathon miezi 10 iliyopita pekee, Kiptum sasa anashikilia nafasi ya tatu bora kati ya sita bora zaidi katika historia ya mbio za masafa marefu.

Wanariadha wengine wanne kwenye orodha hiyo ni Neeraj Chopra wa India, Ryan Crouser wa Marekani, Mondo Duplantis kutoka Sweden, na Noah Lyles wa Marekani.

Watano hao, ambao wanawakilisha nchi nne na vyama vinne vya riadha kutoka mataifa yao, wamefanikiwa kuandikisha maonyesho ya kuvutia katika vitengo mbalimbali vya riadha mwaka 2023.

TRT Afrika