Vifo na Uharibifu kutokana na mafuriko yalishuhudiwa kufuatia mvua kubwa ya takriban siku nzima mnamo Jumapili, Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara, vimezidi huku serikali ya Tanzania ikianzisha operesheni ya kuwafikia waathiriwa.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewaongoza viongozi mbalimbali wa serikali ya Tanzania hadi eneo hilo kupitia helikopta za Jeshi la Wananchi Tanzania ili kutathmini kiwango cha uharibifu ili kubuni suluhu ya haraka huku taifa hilo likiomboleza vifo vya zaidi ya watu 50.
Aidha, taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imesema kwamba serikali italipia gharama zote za mazishi ya wale wote waliopoteza maisha kwenye mafuriko hayo.
Zaidi ya watu 80 waliojeruhiwa, wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya kupata matibabu ya haraka.