Wizara ya Fedha nchini Uganda imetoa Waraka wa pili wa makadirio ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 na kueleza kuwa serikali ina mpango wa kupunguza matumizi yake hadi kufikia dola bilioni 17.9 (Shilingi trilioni 66.065).
Hii ni punguzo la shilingi trilioni 6.049 kutoka bajeti ya 2024/25 ya dola bilioni 19.5 (Shilingi trilioni 72.136).
Wizara ya fedha inaeleza kuwa Mamlaka ya Mapato ya Uganda (URA) inatarajiwa kukusanya zaidi ya dola bilioni 9.6 (shilingi trilioni 35.693) za kodi, kutoka zaidi ya dola bilioni 8.7 ( Shilingi trilioni 32.097) katika mwaka wa fedha wa 2024/25.
Kiwango kinachobaki kitapatikana kwa kukopa na kutoka kwa wafadhili.
Ulipaji wa deni
Wizara ya fedha imeambia kamati ya bunge kuwa sehemu kubwa ya bajeti itaenda kwenye ulipaji wa deni.
Serikali imetenga zaidi ya dola bilioni 2.6 (shilingi trilioni 9.641) kwa ajili ya kulipa deni la ndani ikiwa ni punguzo kutoka zaidi ya dola bilioni 3.2 (shilingi trilioni 12.021) katika bajeti ya sasa.
Zaidi ya dola bilioni 1.1 ( shilingi trilioni 4.287) itaenda kwenye ulipaji wa deni la nje. Hiki ni kiwango cha chini kutoka dola milioni 854 (shilingi trilioni 3.149) mwaka 2024/25.
Aidha, serikali imetenga zaidi ya dola bilioni 3 ( shilingi trilioni 11.191) kwa ajili ya ulipaji wa mikopo ya nje iliyokopwa kugharamia miradi mbalimbali, ikiwa hii ni ongezeko kutoka dola bilioni 2.6 ( shilingi trilioni 9.583) zilizotengwa mwaka 2024/25.
Kwa mikopo iliyopatikana kutoka kwa benki za ndani ya nchi zaidi ya dola bilioni 2.6 (shilingi trilioni 9.641) zimetengwa, kutoka zaidi ya dola bilioni 3.2 ( shilingi trilioni 12.021) katika mwaka wa sasa wa fedha.
Zaidi ya dola milioni 54.2 ( shilingi bilioni 200) pekee ndio zimetengwa kwa ajili ya malipo ambayo hayakamilishwa ya ndani, na ambayo ni zaidi ya dola bilioni 2.7 (shilingi trilioni 10).