Kuhusu TRT Afrika
Kituo cha kidijitali cha TRT ni ukurasa mbadala wa Redio ya Taifa ya Uturuki na shirika la televisheni la TRT – Shirika la utangazaji linaloongoza nchini Uturuki.
Huduma hii ya kidijitali ya TRT Afrika ilianzishwa Machi 2023 kama sehemu ya mpango yenye lengo la kutoa habari za kidijitali kupitia lugha tofauti kutokana na hali halisi ya ongezeko la taarifa tofauti ulimwenguni.
TRT Afrika inafanya kazi kwa kuhusisha jumla ya lugha nne: Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na Hausa.
Kuzinduliwa kwa jukwaa hili ni nyongeza ikizingatiwa kuwa yapo majukwaa mengine ya kidijitali ya TRT yakiwemo: TRT World, TRT Francais, TRT Arabi, TRT Balkan, TRT Russia na TRT Deutsch.
TRT Afrika inawezesha hadhira yake na wafuatiliaji kwa ujumla kwa kuwaleta karibu na uandishi wa habari unaozingatia maadili ya kitaaluma na kuyapa sauti masuala yanayowahusu bila upendeleo.
Hali kadhalika TRT Afrika inazipa sikio taarifa muhimu zenye mashiko katika bara la Afrika hususan zinazopuuzwa na kutopewa kipaumbele.