Kombe la mabingwa Ulaya.  Picha: Reuters

Borussia Dortmund na Paris Saint-Germain wote wana faida ya magoli matatu kila mmoja watakapoingia kwenye mechi zao viwanja mbalimbali. PSV Eindhoven inaingia kwenye mkondo huu ikiwa imefungwa 2-1 na Juventus katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Itakuwa patashika nguo chanika wakati Real Madrid itakapokuwa wenyeji wa Manchester City. Katika mechi ya kwanza Real ilipata ushindi wa 3-2 kwenye uwanja wa nyumbani wa Man City.

Arsenal, Aston Villa, Atletico Madrid, Barcelona, Inter Milan, Leverkusen, Lille na Liverpool tayari wameingia kwenye hatua ya timu 16 baada ya kumaliza miongoni mwa nane bora kwenye ligi hiyo.

Droo ya hatua ya timu 16, itafanyika Ijumaa Februari 21. Mechi za hatua hiyo zitaanza kuchezwa 4/5 Machi na mkondo wa pili kurindima wiki inayofuatwa.

Reuters