Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba amesema kuwa noti mpya za Tanzania zenye saini ya Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba na yeye mwenyewe zitaingia kwenye mzunguko kuanzia Februari 1, 2025.
Kulingana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emanuel Tutuba, noti mpya za Tanzania zitaingia kwenye mzunguko wa fedha kuanzia tarehe Februari 1, 2025.
Noti hizo zenye saini ya Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Mwigulu Nchemba na Gavana Tutuba ni za toleo la mwaka 2010.
Noti hizo zitatumika sambamba na noti zilizopo hivi sasa huku zikiwa zina mwonekano wa noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, lakini zitakuwa na marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, ” aliongeza Gavana huyo.