Machafuko ya uchaguzi nchini  Msumbiji yameathiri njia kuu ya biashara na Afrika Kusini / Picha: Reuters

Afrika Kusini ilitangaza kusitisha kuingia kwa malori katika kivuko cha mpaka cha Lebombo na Msumbiji kuanzia Jumanne kutokana na wasiwasi wa kiusalama.

Msumbiji imekuwa na maandamano makubwa tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba wakati mamlaka ya uchaguzi ilipomtangaza Daniel Chapo, mgombea urais wa chama tawala, mshindi katika kura iliyozozaniwa ya mwezi Oktoba baada ya madai ya wizi wa kura.

Baraza la Katiba, mahakama ya juu zaidi nchini, ilithibitisha Jumatatu matokeo ya uchaguzi ambayo yaliongeza utawala wa chama cha Frelimo madarakani kwa nusu karne.

Mamlaka ya Usimamizi wa Mipaka ya Afrika Kusini (BMA) imesema kusimamishwa kwa trafiki ya malori kutaendelea "hadi tutakapopewa hakikisho kwamba ukanda huo unalindwa na wanajeshi pamoja na polisi wa upande wa Msumbiji," Kamishna wa BMA Mike Masiapato amenukuliwa katika mahaojiano na mtangazaji wa SABC.

Magari madogo

Mamlakia hiyo imesema ni magari madogo tu na watu wataruhusiwa kuvuka mpaka na kuingia Msumbiji.

Aidha imesema uamuzi huo ulifanywa kabla ya tamko la Baraza la Katiba la Msumbiji.

Lebombo ndio kivuko kikuu cha mpaka cha usafirishaji wa bidhaa na mizigo kati ya nchi hizo mbili.

Mwezi uliopita Afrika Kusini ilitangaza kufungwa kwa muda kwa kivuko cha mpaka chenye shughuli nyingi kutokana na ghasia zinazoendelea baada ya uchaguzi nchini Msumbiji.

TRT Afrika