Mnamo mwaka wa 2017, kampuni hiyo ilikuwa na wafanyikazi wapatao 3,000.  / Picha: AFP

Kampuni kubwa ya kusikiliza mziki kupitia mtandaoni Spotify imesema kuwa itapunguza idadi ya wafanyakazi wake kwa takriban asilimia 17 katika jitihada za kupunguza gharama huku kukiwa na kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi.

Mnamo mwezi Oktoba mwaka huu, Spotify ilichapisha faida adimu ya uendeshaji ya robo mwaka ya euro milioni 32, ikilinganishwa na hasara ya milioni 228 kwa kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita, kufuatia ukuaji wa 26% kwa watumiaji kwa robo tatu.

"Ninatambua kwamba kwa wengi, kupunguzwa kwa ukubwa huu utaleta mshangao mkubwa kutokana na ripoti ya mapato ya hivi karibuni na utendaji wetu," mtendaji Mkuu Daniel Ek aliandika katika barua kwa wafanyakazi, ambayo ilionekana na AFP.

Daniel Ek alisema kuwa mnamo 2020 na 2021, kampuni hiyo "ilitumia fursa iliyowasilishwa na mtaji wa gharama nafuu na kuwekeza sana katika upanuzi wa timu, uboreshaji wa yaliyomo, uuzaji na wima mpya."

"Hata hivyo, sasa tunajikuta katika mazingira tofauti sana. Na licha ya juhudi zetu za kupunguza gharama mwaka huu uliopita, muundo wetu wa gharama ambapo tunahitaji kuwa bado ni mkubwa sana."

Spotify imewekeza sana tangu uzinduzi wake ili kupiga jeki upanuzi katika masoko mapya na, katika miaka ya baadaye, maudhui ya kipekee kama vile podcasts.

Imewekeza zaidi ya dola bilioni moja katika podcast pekee.

Kampuni hiyo haijawahi kuchapisha faida ya mwaka mzima na imekuwa tu ikichapisha mara kwa mara, faida ya robo mwaka, licha ya mafanikio yake katika soko la muziki.

AFP