Uamuzi huo ulitangazwa na Februari 10 na Waziri wa Fedha na Mipango wa nchi hiyo Yusuf Murangwa./Picha:  @yusuf_murangwa   

Serikali ya Rwanda imeanza mchakato wa kuanza kutoza tozo kwenye huduma za kidijiti kama vile Netflix na Amazon.

Uamuzi huo ulitangazwa Februari 10 na Waziri wa Fedha na Mipango wa nchi hiyo Yusuf Murangwa.

“Wanyarwanda wengi hutumia teknolojia za nje kama vile Netflix na Amazon. Tumekubaliana kuwa kuanzia sasa, huduma hizi zitatozwa kodi,” alisema Murangwa katika mahojiano yake na shirika la habari la nchi hiyo.

Inaaminika kuwa, makampuni makubwa, yanayohusisha manunuzi ya kimtandao hutengeneza fedha nyingi kutokana na wigo wa wateja wake ambao umeenea sehemu nyingi ulimwenguni.

Kampuni ya Amazon, ambayo ilianzishwa mwaka 1994 na Jeff Bezos huko Washington nchini Marekani, ikijihusisha na uuzaji na ununuzi wa vitu mbalimbali duniani, wakati Netflix ni kampuni ya Marekani inayotoa huduma ya kutazama filamu na vipindi vya runinga kwa njia za intaneti.

TRT Afrika