Mkutano wa Nne wa Biashara na Uchumi kati ya Uturuki na Afrika umeanza Ahamisi katika mji mkuu wa Uturuki wa Istanbul na utaendelea hadi Oktoba 13.
Wizara ya Biashara wa Uturuki Omer Bolat na Kamishna wa maendeleo ya Kiuchumi, biashara, viwanda, na madini katika Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Albert Muchanga na rais wa bodi ya uhusiano wa nje ya uturuki DEIK Nail Olpak ni miongoni mwa wakuu walioshiriki ufunguzi wa mkutano huo siku ya alhamisi.
Mkutano huo wa siku mbili, ulioandaliwa na bodi ya uhusiano wa nje ya uturuki (DEIK) kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara na Jumuiya ya Afrika, imewatua washiriki 3,000 wakiwemo wakuu wa sekta ya Kibiashara barani Afrika.
Mkutano huo wenye kauli mbiu, "Kushughulikia changamoto, Kufungua fursa: Kujenga Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Uturuki na Afrika", unatanguliza sekta za nishati, miundombinu, kilimo, biashara ya kilimo, huduma za afya, utalii, na uuzaji wa dijitali.
Kiwango cha biashara kati ya Uturuki na Afrika kilifikia dola bilioni 40.7 mnamo 2022 ikiwa ni ongezeko kutoka dola bilioni 1.35 mnamo 2003. Takwimu hiyo inakadiriwa kufika hadi dola bilioni 50 mwishoni mwa mwaka huu.
Katika siku ya pili ya mkutano huo, wafanyabiashara wa kituruki na wa Afrika watachangia uzoefu wao katika kuunda upya mazingira ya ulimwengu wa biashara wakati wa Mazungumzo ya Uongozi wa Wanawake wa Uturuki na Afrika.