Harambee Stars wakiwa mazoezini mjini Nairobi: Picha Shirikisho la Soka la Kenya

Harambee Stars ilianza mazoezi yake Jumamosi, kufuatia kuwasili kwa wachezaji wanaocheza ughaibuni wakiongozwa na Michael Olunga.

Wachezaji hao wanaoendelea na mazoez kambini chini ya kocha Engin Firat, watazidi kujinoa kwa muda ya siku mbili kabla ya kufunga safari kuelekea Gabon siku ya Jumatano Novemba 15, 2023.

Kenya inatarajiwa kuwa na kibarua kigumu kwenye Kundi F la katika michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia FIFA 2026 kwani imepangwa pamoja na Côte D'ivoire, Gabon, Gambia, Burundi, na Ushelisheli.

Timu hiyo itakipiga ugenini mfululizo dhidi ya Gabon Alhamisi hii, Franceville, kabla ya kuminyana na Ushelisheli Abidjan, Ivory Coast, Jumatatu, Novemba 20, 2023.

Kikosi cha awali cha wachezaji 28 kilichotajwa na mkufunzi wa Harambee Stars Engin Firat kwa minajili ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA 2026 dhidi ya Gabon na Ushelisheli.

Walindalango

Patrick Matasi (Kenya Police), Ian Otieno (Zesco), Joseph Ochuka (Bandari)

Mabeki

Nabi Kibunguchy (Orlando City), Hanif Wesonga (KCB), Abud Omar (Kenya Police), Daniel Sakari (Tusker), Geoffrey Ochieng (Gor Mahia), Daniel Anyembe (Viborg), Eric Ouma (AIK), Joseph Okumu (Reims), Johnstone Omurwa (CF Estrela), Amos Nondi (Ararat)

Viungo

Duncan Otieno (Gaborone United), Teddy Akumu (Sagan Tosu), Duke Abuya (Singida), Ayub Masika (Nanjing City), Kenneth Muguna (Kenya Police), Eric Balecho (Murang Seal), Rooney Onyango (Gor Mahia), Eric Johanna (UTA ARAD), Richard Odada (Aalborg), Alfred Scriven (Hodd) na Timothy Ouma (Elfsborg)

Washambuliaji

Masud Juma (Al Faisaly), Michael Olunga (Al Duhail), Moses Shummah (Kakamega Homeboyz) na Benson Omalla (Gor Mahia)

TRT Afrika