Kenya imejumuishwa iki Kundi F pamoja na Côte D'ivoire, Gabon, Gambia, Burundi, na Seychelles hatua ya makundi ya kufuzu kombe la Dunia la FIFA 2026. Picha: Getty

Kikosi cha Harambee Stars kikiongozwa na kocha Engin Firat kimetua Franceville, Gabon tayari kukwatuana na wenyeji hao.

Kenya imejumuishwa pamoja na Côte D'ivoire, Gabon, Gambia, Burundi, na Shelisheli katika Kundi F kwenye michuano ya makundi ya kufuzu kombe la Dunia la FIFA 2026.

Engin Firat amekipunguza kikosi cha awali cha wachezaji 28 alichokitaja hadi wachezaji 21.

Baada ya Gabon, Kenya itaelekea hadi mji wa Abidjan, Côte D'ivoire kukabiliana na Ushelisheli katika mechi yake ya pili ya kufuzu itakayopigwa Jumatatu, Novemba 20, 2023, katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny ulioko Abidjan.

Kikosi cha Harambee Stars kilichosafiri kuelekea Gabon

Patrick Matasi (Kenya Police), Ian Otieno (Zesco), Joseph Ochuka (Bandari), Daniel Sakari, Dennis Nganga, Johnstone Omurwa, Abud Omar, Amos Nondi, Eric Ouma, Nabi Kibunguchy, Haniff Wesonga.

Wengine ni pamoja na Ayub Masika, Alfred Scriven, Duke Abuya, Rooney Onyango, Duncan Otieno, Richard Odada, Kenneth Muguna, Anthony Akumu, Timothy Ouma, Eric Johanna, Masud Juma, Michael Olunga, na Benson Omala.

Waamuzi wa mechi hiyo ya Kufuzu kwa Kombe la Dunia la Harambee Stars na Gabon wataongozwa na refa mkuu Mansour Mohammed, akisaidiwa na mwamuzi msaidizi wa kwanza Gamal Saad, Abdelfattah Elsnadidy kama mwamuzi msaidizi wa pili na Adel Hussein kama afisa wa nne.

TRT Afrika