Jioni ya Jumatano (Novemba 15) katika vyumba vya kubadilishia nguo vya Uwanja wa El Abdi huko Morocco, wachezaji wa Ethiopia na Sierra Leone walijiandaa kwa mchezo muhimu wa kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026, bila kujua hali ya hewa kama ingebadilika
Baada ya dakika tano za mchezo, ukungu mdogo ulianza kuonekana, lakini mchezo uliendelea bila kusimamishwa, huku timu zote zikijiandaa kuchukua ushindi katika mechi hiyo.
Hata hivyo, mchezo ulipofikia dakika ya 30, ilikuwa wazi kuwa kutakuwa na matatizo ya hali ya hewa.
Ukungu mzito ulishuka na kuzingira uwanja, na Shirikisho la Soka la Ethiopia likaposti picha kwenye mitandao ya kijamii ya wachezaji wakicheza huku uwezo wa kuona ukiwa mdogo sana.
Mapumziko ya nusu muda yalitangazwa, na wakati wachezaji waliporudi vyumbani mwao, FIFA na maofisa wa mechi walionekana uwanjani wakijaribu kufanya maamuzi muhimu kuhusu jinsi ya kuendelea na mchezo.
Hata hivyo, mashabiki wanaotazama mchezo nyumbani walipata wasiwasi wakati mapumziko ya dakika 15 yalipomalizika na wachezaji hawakutokea uwanjani.
Lakini Hali ya faraja na furaha ilitanda mitandaoni wakati mchezo ulipoendelea baada ya saa moja ya mashabiki kutazama mchezo nyumbani Ethiopia na Sierra Leone.
"Habari njema! Mchezo umeanza tena rasmi... Uwezo wa kuona kwa wachezaji umerejea baada ya ukungu kupungua" alitangaza shabiki mmoja aliyejawa na msisimko mkubwa kufuatilia mtanange huo, @negussu, kwenye X.
Waamuzi waliendelea na kusitisha mchezo mara mbili kipindi cha pili kabla ya mchezo kumalizika baada ya dakika 15 za muda wa kawaida.
Wachezaji waliokuwa wamechoka pande zote walizungumza baada ya mchezo lakini hawakulaumu moja kwa moja hali ya hewa kwa matokeo.
Sierra Leone itacheza na Misri Novemba 19 na Ethiopia itakutana na Burkina Faso Novemba 21.