Mashindano mengine ya kimataifa ya soka, Afcon, yameisha, na wenyeji Cote D’ivoire wameinyanyua kombe baada ya fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa katika fainali na Nigeria.
Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies lilianza huko Abidjan, Côte d’Ivoire tarehe 13 Januari. Katika mwezi unaaofuata, timu za taifa 24 zilishindana kwa taji lenye hadhi kubwa zaidi barani. Kampuni kimekuwa kikidhamini mashindano haya kwa muda sasa, ukarimu wake ukiwafanya watu kusahau upande mwingine wa biashara yao ambayo huonekana kutotanguliza masilahi ya waafrika.
Katika Afrika Mashariki mwaka 2023, wakazi wanaoishi karibu na njia ya mradi wao wa EACOP – bomba la mafuta linalotoka magharibi mwa Uganda hadi mashariki mwa Tanzania – wanasema wamenyang'anywa ardhi na njia zao za kujikimu. Taasisi za Uwajibikaji wa mabadiliko ya tabia nchi zinakadiria kuwa bomba hilo litasababisha uchafuzi wa hewa wa kaboni mara 25 zaidi ya utoaji wa gesi wa kila mwaka,ukijumlisha Uganda na Tanzania kwa hesabu za sasa.
Mashtaka yasiyoisha
Mahakama ya Afrika Mashariki ilikataa kusikiliza changamoto ya kisheria dhidi ya TotalEnergies iliyowasilishwa na vikundi vya mazingira, kwa misingi kwamba ilifunguliwa kwa kuchelewa sana, lakini vikundi hivyo vinaendelea kuwa sauti katika wito wao wa kampuni hiyo kususiwa.
Oktoba 2023; malalamiko ya jinai ya mauaji yalifunguliwa nchini Ufaransa dhidi ya TotalEnergies na manusura na wanafamilia wa wahanga wa shambulio la kigaidi la 2021 huko Cabo Delgado, Msumbiji karibu na mradi wao wa gesi asilia wa dola bilioni 20.
Rasmi, idadi ya vifo iliripotiwa kuwa katika makumi lakini waandishi waligundua kuwa watu 1,200 huenda walifariki katika shambulio hilo. Katika mashtaka ya mahakama, manusura na jamaa wa wahanga wanaishtaki Total kwa kutofuata hatua zinazohitajika kulinda wakandarasi na kwa makusudi kutoa msaada kwa watu walio hatarini. Total imekana tuhuma zote.
Lakini inaweza kuwa vigumu kusikia wito kama huo juu ya vigelegele vya umati wa watu, kwa hivyo sio vigumu kuelewa kwa nini kusafisha taswira ya mtu kwa kudhamini michezo.
Zaire ilivyotumia njia ya masumbwi kuficha maovu
Mfano mzuri kuliko yote Afrika, na labda yenye mafanikio zaidi wa - mtu kujisafisha madudu yake - ulikuwa ni pambano la ndondi la "Rumble in the Jungle" la mwaka 1974. Kiongozi wa Zaire, DRC ya zamani, Mobutu Sese Seko alijaza mifuko ya wapromota wa ndondi ili kuandaa pambano kati ya Wamarekani weusi maarufu wa masumbwi, Muhammad Ali na George Foreman.
Utawala wa Mobutu ulipindua na kumuua Patrice Lumumba, kiongozi wa kupinga ukoloni, hali iliyowakasirisha viongozi wa haki za kiraia waliokuwa wanamheshimu Lumumba, na akatafuta kurudisha upendeleo kwao.
Total ilifadhili baadhi ya mikutano ya mabadiliko ya tabianchi mwaka jana nchini Kenya na COP 28 katika Falme za kiarabu pia.
Lakini hatupaswi kamwe kusahau kwamba zoezi la kampuni au mtu kujisafisha wakati wa matukio makubwa ya kidunia ni zana ya kijanja inayosafishwa katika michezo tunayoipenda.
Hatari hizi ni sawa mikononi mwa kiongozi fisadi kama ilivyo kwa kampuni ya kimataifa.