Kwanini Mjadala ni mkubwa juu ya bandari?

Na Nuri Aden na Gaure Mdee

Ubinafsishaji wa bandari au uendeshaji wa baadhi ya maeneo ya bandari umekuwa ni mfumo uliopata umaarufu hivi karibuni, lakini mifumo hiyo imezua mjadala mkubwa baada ya kufika Afrika Mashariki.

Bandari ni sehemu muhimu ya mwingiliano wa kibiashara za kimataifa. Mara nyingi, hutumika kama njia kuu za kuunganisha mataifa mbalimbali huku pia zikitoa huduma za usafirishaji wa bidhaa na malighafi. Bila bandari, sehemu kubwa ya uchumi wa dunia ingekwama.

Bandari zilizopo katika eneo la Bahari ya Hindi na Bahari Nyekundu ni njia kuu za biashara na mnyororo wa usambazaji wa kimataifa. Zipo katika njia za usambazaji wa mafuta na gesi na kwenye sehemu ya mpango ya njia mpya za biashara inayo buniwa na China inayojulikana kama “Belt & Road.”

Licha ya Afrika kubarikiwa na mali ghafi tele, na nchi nyingi za Afrika kuwa na miundombinu ya bandari, uendeshaji na ufanisi wa bandari hizo umekuwa tatizo kutokana na ukosefu wa vifaa vya kisasa licha ya kuwa na faida ya kijiografia.

Bandari 10 kubwa zaidi duniani zinapatikana tatu zikiwemo China, Singapore na Uholanzi.

Ni kutokana na hali hiyo, ndio imekuwa kichocheo kikubwa kwa nchi na mashirika yenye nyenzo na uzoefu mkubwa wa kuendesha bandari kama Singapore, Uholanzi, na China imefanya iwe rahisi kwa waendeshaji wa kigeni kupata mikataba katika nchi ambazo zinatatizikia kuendesha na kuendeleza bandari zao.

Mataifa mbalimbali kama China, Ulaya na Marekani kupitia mashirikia ya kusimamia bandari, ni wawekezaji wakubwa wa bandari Afrika. 

Changamoto zimetapakaa

Bandari za Tanzania na Kenya zinakabiliwa na changamoto zinazofanana kama vile msongamano, miundombinu iliyopitwa na wakati, na ushindani mkubwa kutoka kwa bandari nyingine katika eneo hilo.

Bandari za kisasa zinahitaji uwezo wa kufikia uchumi wa hali ya juu (economies of scale) na kuhudumia meli zenye makontena makubwa ambazo zinaathiri sana biashara ya kimataifa. Kimsingi, huwezi kuwa kitovu kikuu cha biashara na vifaa bila miundombinu na uendeshaji wa bandari kubwa.

Nchi za Kiafrika pia zinafungua milango kwa uwekezaji wa ubinafsishaji ambao utanufaisha wawekezaji na wamiliki.

Ubinafsishaji unapojitokeza - Vita za bandari, Kenya na Tanzania

Mapambano ya nchi za Afrika Mashariki kumiliki bandari ya kikanda yalifikia hadi hatua ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuelezea kwa njia yake mwenyewe kuwa mkataba wa ubinafsishaji ulikuwa mzuri kwa sababu "jirani", pia, alikuwa ana azma sawa, na pia alikuwa akiwapa bandari nyingi zaidi kuliko Tanzania hivyo mkataba ilibidi uharakishwe

"Wenzetu kwa kuona malumbano yetu, mmeona, wameruka wameenda kule kule Na lile lile jumba lililowekwa bendera ya Tanzania. limekwekwa bendera ya jirani. Sasa Tanzania tumeuza, wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?," rais Samia alisema

Takriban asilimia 95 ya biashara ya kimataifa ya baharini ya Tanzania inashughulikiwa katika bandari ya Dar es Salaam. Bandari hiyo inahudumia nchi sita zisizo na pwani ikiwemo Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda, na DRC ya Mashariki.

Bandari Kavu ya Rwanda iliyoshughulikiwa na mwekezaji wa nje

Mbali na Tanzania, nchini Kenya, ilidaiwa kuwa mkataba uliotiwa saini na mwekezaji binafsi wa kigeni, ungewaruhusu kusimamia vituo vya Mamlaka ya Bandari yani Kenya Ports Authority, ikiwemo bandari mpya ya Lamu.

Madai hayo dhidi ya bandari hiyo ya Mombasa, yaliibua hisia na kuzua mjadala mkubwa kutokana na umuhimu wake, kwani, mbali na kuhudumia Kenya, pia inahudumia nchi kadhaa kama vile Uganda, Burundi, Rwanda, Kongo ya Mashariki, Sudan Kusini na Ethiopia.

Bandari hiyo pia inahudumia nchi sita zisizo na pwani ikiwemo Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda, na DRC ya Mashariki

Bandari ya Mombasa nchini Kenya. Picha: Mamlaka ya Bandari Kenya

Inaunganishwa moja kwa moja na bandari muhimu za Ulaya Magharibi, Asia, Amerika na nchi za Mashariki.

Hata hivyo, mipango ya ubinafsishaji huo ilipingwa vikali kabla ya uchaguzi, ingawa serikali tayari ilikuwa imekubaliana mwekezaji asiyetajwa dhidi ya kampuni nyingine katika makubaliano kati ya mataifa hayo mawili.

Mkataba ulikuwa umepangwa kutekelezwa mwezi Julai 2022, na serikali ilihitajika kutoa ombi la mapendekezo kabla ya Uchaguzi wa Agosti 2022 na ungewaruhusu wawekezaji kusimamia vituo vya Mamlaka ya Bandari yani Kenya Ports Authority, ikiwemo bandari mpya ya Lamu.

Nchi sasa imerudi kujadili makubaliano mapya hivi karibuni.

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir pamoja na Gavana wa zamani Hassan Joho na viongozi wa Pwani wamehusika sana katika mjadala wa bandari Kenya | Picha: Aisha Jumwa

Nchi sasa imerudi kujadili makubaliano mapya hivi karibuni.

Dhamira za wawekezaji kutoka nje

Kwa muda mrefu, kumekuwa na dhamira ya kuendesha bandari Kusini, Mashariki na Pembe ya Afrika, ikiwa ni pamoja na Msumbiji, Tanzania, Kenya, Somalia, Eritrea na Djibouti.

Nchi nyingi za kimataifa zimefanikisha ndoto zao za kuendesha bandari barani Afrika ikiwemo China inayoendesha bandari 12 Afrika. Mataifa mengine pia yanaendesha bandari mbali mbali duniani huku baadhi ya hao waendeshaji wakubwa wa kimataifa wakielekeza macho yao katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Aidha, baadhi yao yemeanzisha pia bandari kavu mfano ikiwa ni bandari iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambacho ni ni kituo kikubwa cha kushughulikia mizigo nchini humo.

Hata hivyo, licha ya ufanisi na uzoefu wa muda mrefu wa mataifa ya kigeni katika kuendesha bandari kisasa zaidi, hivi karibuni, miradi ya ubinafsishaji imekumbana na upinzani kutoka asasi za kiraia na wanasiasa katika nchi za Afrika Mashariki baada ya kukosolewa kutokana na kasoro katika vipengele kadhaa vya kisheria.

Nchini Tanzania, - Kwa pendekezo la kuchukua uendeshaji wa bandari kuu ya Dar es Salaam na kurudi kuchora upya mipango, wawekezaji wa kigeni walichukuliwa kama vikwazo wakati vipengele vya makubaliano vilidaiwa kufichwa kutoka kwa umma na ukosoaji mkubwa ulitolewa kuhusu kampuni hiyo na biashara zake.

Kesi mbalimbali zimeanzishwa nchini Tanzania juu ya usiri wa makubaliano kwenye mkataba wa DP | Picha: Getty

Hatua hii inakuja baada ya serikali kusema imefanya marekebisho katika baadhi ya vipengele vilivyokuwa vikilalamikiwa mwanzoni, baadhi ya marekebisho hayo ni pamoja na serikali kuchukua 60% ya mapata au faida, na pia utaratibu wa kukagua kazi na utekelezaji wa mkataba kila baada ya miaka mitano.

Nchi nyingine katika mbio za bandari za Afrika Mashariki ni pamoja na Ufaransa.

Waendeshaji wa Kifaransa kutoka kundi la Bollore wana lalamikiwa kuhusu jinsi walivyopata mikataba katika kupata udhibiti wa bandari zao, wakiuza tawi lao kubwa la Usafirishaji wa Kiafrika kwa MSC huko Afrika Magharibi na bado kuwa wakubwa zaidi katika mchezo wa usafirishaji na bandari upande huo wa bara.

Nchini Tanzania hivi karibuni - Septemba mwaka huu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeikabidhi Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL) hio hio ya Ufaransa, kuendesha na kusimamia bandari ya Malindi kutoka Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC), kwa lengo la kuongeza mapato na ufanisi katika visiwa.

Inakadiriwa gharama ya kujenga bandari hiyo ni USD 220,000 na ZPC watapata asilimia 30 ya mapato yatakayopatikana.

Aboubaker Omar Hadi, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Bandari na Maeneo Huru ya Djibouti (DPFZA), katika bandari ya Doraleh Multi-purpose Port (DMP), Djibouti. | Picha: Getty

Hatua hii inakuja baada ya serikali kusema imefanya marekebisho katika baadhi ya vipengele vilivyokuwa vikilalamikiwa mwanzoni, baadhi ya marekebisho hayo ni pamoja na serikali kuchukua 60% ya mapata au faida, na pia utaratibu wa kukagua kazi na utekelezaji wa mkataba kila baada ya miaka mitano.

Bandari kubwa za Afrika Mashariki zina uwezo ufuatao katika mizani ya TEU; Twenty Foot Equivalents yaani makasha ya kusafarisha bidhaa ya futi 20

● Dar es Salaam ~700,000

● Mombasa ~ 1,400,000

Kulinganisha na bandari nyengine duniani

● Shanghai ~47,000,000

● Singapore ~37,000,000

● Jebel Ali ~14,000,000

Ili kuweka hili katika mtazamo halisi, tunalinganisha uwezo wa Shanghai:

Shanghai kwa siku 5, Dar inashughulikia kwa mwaka, Shanghai kwa siku 10, Mombasa inashughulikia kwa mwaka

Wawekezaji wengine barani

Jengo laofisi la vifaa vya Bollore, Africa Group logistics | Picha: Getty

Waendeshaji wa Kifaransa kutoka kundi la Bollore, yani Africa Group Logistics wana lalamikiwa kuhusu jinsi walivyopata mikataba katika kupata udhibiti wa bandari zao, wakiuza tawi lao kubwa la Usafirishaji wa Kiafrika kwa MSC huko Afrika Magharibi na bado kuwa wakubwa zaidi katika mchezo wa usafirishaji na bandari upande huo wa bara.

Inakadiriwa gharama ya kujenga bandari hiyo ni USD 220,000 na ZPC watapata asilimia 30 ya mapato yatakayopatikana.

Uchumi wa kiwango na mkusanyiko zinachangia kuweka waendeshaji wa ndani kwenye hasara kubwa. Waendeshaji wakubwa wa bandari tayari wana mahusiano na meli zakutosha, wanaelewa mazingira na wana ufadhili wa kifedha.

Kwa upande mwingine, kimkakati, nchi zinaweza haraka kuwa vitovu vya usafirishaji kwa kufaidi kupitia baadhi ya hizi faida na uzoefu kutoka kwa wawekezaji hawa.

Morocco, Tangier: eneo la bandari na kituo cha feri. | Picha: Getty

Katika bandari kubwa 50 duniani, ni Tanger (Morocco) peke yake ndio ipo barani Afrika. Hii ni ishara tosha kuwa Afrika iko nyuma katika miundombinu inayoipa nguvu ya kibiashara ya kimataifa

Swali mwisho wa siku ni, nchi za Kiafrika zifanyaje kuboresha matarajio yao ya kibiashara?

TRT Afrika