Serikali ya Kenya na Uganda imetoa tahadhari kwa raia wake juu ya hatua zitakazochukuliwa siku chache zijazo baada ya Tanzania kutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Marburg katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa nchi na kupelekea vifo vya watu watano.
Uganda inapanga kutuma timu ya kutathmini hatari katika wilaya na mpaka wa Kasensero na Mutukula.
Wizara ya Afya nchini Uganda imetangaza kutuma kikosi cha kuwapima na kuwachunguza watu wanaoishi kwenye mpaka kati ya Uganda na Tanzania kwa nia ya kuhakiki virusi vya Marburg kuvuka mpaka.
Kwa mujibu wa tangazo la Waziri wa Afya Tanzania mwanzoni mwa wiki hii, Jumla ya watu 161 waliobainika kuwa hatarini kupata madhara na waliokufa na wanaopatiwa matibabu tayari wametambuliwa na wanafuatiliwa kwa karibu.
Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Afya, Dkt Henry Mwebesa, katika taarifa yake kwa viongozi wote wa Wilaya, alisema inabidi wafanye ufuatiliaji wa mpaka juu ya suala hilo na kuhakikisha kwamba linadhibitiwa.
Uganda ina uzoefu mkubwa wa kudhibiti MVD, kwani walikuwa na mlipuko mwishoni mwa 2017.
Majirani wakiwa katika tahadhari kubwa
Nchi jirani ya Kenya imeweka wazi kwamba kwa kuwa huu ni nchi jirani, kutakuwa na uchunguzi wa kina kwa wageni wanaokuja nchini na miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya.
Wakenya wamechukua hatua sawa ili kukabiliana na kizuizi kama Uganda ilivyochukua.
Katika ukurasa wa Twitter ya Wizara ya Afya Kenya, serikali ilisema kwamba Vivuko vya Bukoba na Uwanja wa Ndege vimeangaziwa kama maeneo ambayo yatafanyiwa uchunguzi, na kutakuwa na utaratibu wa ufuatiliaji na majibu katika mipaka mbalimbali kati ya Kenya, Uganda na Tanzania.
Kwa sasa hakuna chanjo au matibabu yaliyoidhinishwa kutibu Marburg. Kurejesha maji mwilini kwa vimiminika vya kumeza na kwa mishipa (invitro) na matibabu ya dalili kadhaa huongeza uwezekano wa kuishi.
Shirika la Afya Duniani litaisaidia Wizara ya Afya nchini Tanzania kwa kupeleka timu ya dharura mkoani Kagera kufanya uchunguzi zaidi. Timu ya dharura itazingatia kesi zinazoendelea katika maeneo ya karibu na vituo vya afya vya ili kutambua waliobainika kuwa hatarini kuambukizwa zaidi na kuwapa huduma inayofaa.