Baadhi ya ndugu na jamaa wa waathirka wa shambulio hilo wakiwakumbuka wapendwa wao./Picha: X Ubalozi wa Marekani-Kenya

Kenya na Tanzania zimeadhimisha miaka 26 toka kutokea kwa shambulizi la bomu la kujitoa mhanga katika balozi za Marekani mjini Nairobi na Dar es Salaam, yalioa zaidi ya watu 224 na kujeruhi zaidi ya 4,000.

Mbali na vifo, shambulio hilo lilisababisha uharibu mkubwa wa miondumbinu, yakiwemo majengo ya ubalozi huo.

Kikundi cha Al Qaeda kilidai kuhusika na milipuko hiyo pacha, ambayo yaliua raia wengi kutoka Tanzania na Kenya.

Mnamo Agosti 7, 1998, majira ya nne na dakika thelathini na tisa asubuhi, gari lililokuwa mabomu lililipuka katika balozi mbili za Marekani nchini Kenya na Tanzania, kwa wakati mmoja.

Wakati watu 212 walipoteza maisha na wengine 4,000 kujeruhiwa mjini Nairobi, jijini Dar es Salaam, watu 11 waliripotiwa kuuwawa na wengine 85 kujeruhiwa katika tukio hilo.

Kati ya waliopoteza maisha katika tukio hilo, 56 walikuwa ni wafanyakazi walikuwa ni raia wa Marekani.

Mnamo Agosti 7, 1998, majira ya nne na dakika thelathini na tisa asubuhi, gari lililokuwa mabomu lililipuka katika balozi mbili za Marekani nchini Kenya na Tanzania, kwa wakati mmoja./Picha: Wengine

Wengi waliopoteza maisha ni raia wa Kenya na Tanzania huku simulizi mbalimbali za vitabu na filamu zikiwa zimetungwa kufuatia tukio hilo.

Kumbukumbu yenye majina ya waathirika wa mlipuko wa jijini Nairobi./Picha: Getty

Jijini Dar es Salaam, magaidi waliokuwa wanaendesha lori lililosheheni mabomu, waligonga geti la ubalozi, wakapiga risasi maofisa wa ubalozi huo.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Meg Whitman akishiriki kumbukumbu hiyo./Picha: X Ubalozi wa Marekani Kenya

Jijini Dar es Salaam, asubuhi majira ya saa 4, gari lililobeba mabomu hayo liliendeshwa kupitia barabara ya Laibon ulipokuwepo Ubalozi wa Marekani kuelekea moja kati ya mageti mawili ya Ubalozi huo na kulipuka majira ya 4 na dakika 39.

Majengo ya Ubalozi yaliharibiwa vibaya na kupelekea kutotumika tena, baadhi ya majengo ya Karibu pia yaliharibiwa vibaya yakiwemo Balozi za Ufaransa na Ujerumani ambazo zilikua Karibu na eneo hilo pia ziliharibiwa na mlipuko huo lakini hakuna aliejeruhiwa.

Ubalozi wa Marekani ulihamia katika majengo hayo ambayo yaliyokua Ubalozi wa Israel, mnamo Mwezi Mei 1980 ambayo yalijengwa miaka ya 1970.

TRT Afrika
Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuziSera ya Vidakuzi
Kubali