Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Dkt. Ashatu Kijaji na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Güllüoğlu

Mkutano huo uliongozwa na Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, uliandaliwa na Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania.

Wafanyabiashara wa Uturuki wanaowakilisha sekta za teknolojia, ujenzi na mavazi, walikutana na wafanyabiashara wenzao kutoka zaidi ya makampuni 100 za Tanzania ili kubadilishana mawazo na jinsi ya kufanya biashara pamoja.

"Katika kipindi cha miaka 26 iliyopita, biashara baina ya nchi hizo mbili ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa huku mauzo ya nje kutoka Uturuki kwenda Tanzania yameongezeka kwa kiwango cha asilimia 17.3 kila mwaka kutoka dola milioni $4.55 mnamo 1995 hadi dola milioni 500 2022," Waziri alisema.

Kwa upande wake, Balozi wa Uturuki Tanzania, Mehmet Gulluoglu, alisema kuwa nchi hizo zina matarajio ya mafanikio makubwa kutokana na uhusiano mkubwa kati ya mataifa hayo mawili.

"Tanzania na Uturuki sio washindani wa biashara bali, sisi sote ni washirika ambao tumekuwa tukisaidiana kuimarisha biashara mbalimbali kwa Watanzania kupeleka bidhaa nchini Uturuki na vile vile kwa upande wa Uturuki," alisema.

Vile vile, mnamo 2021 Tanzania ilisafirisha bidhaa zenye thamani ya dola milioni 37.6, hadi Uturuki, haswa dhahabu yenye thamani ya dola milioni $14.9 na tumbaku mbichi yenye thamani ya dola milioni 11.2.

Waziri wa Biashara Ashatu alisema kuwa Tanzania na Uturuki ziko na uhusiano wa kihistoria na kukua kwa kiwango na sera zinazopanuka huku mipango ya kifedha ikifanikiwa katika kupelekea usawa wa mapato na ufanisi wa kibiashara wa nchi hizo.

Mataifa hayo mawili yalijadili ukuzaji wa biashara kati yao huku wengi wa wafanyibiashara kutoka Tanzania chini ya miamvuli ya Baraza la Biashara, Viwanda na Kilimo cha Tanzania (TCCIA), Shirikisho la Viwanda la Tanzania (CTI), Baraza la Biashara la Wanawake Tanzania (TWCC) na Shirika la Sekta Binafsi la Tanzania (TPSF).

Aidha, ufanisi wa biashara kati ya mataifa hayo umechangiwa na Shirika la Ndege la Uturuki, Turkish Airlines kwa kufungua kwa kuanzisha safari za moja kwa moja kutoka Istanbul hadi Dar es Salaam na Zanzibar mara tatu kwa wiki.

Kampuni maarufu ya ujenzi ya Uturuki Yapı Merkezi imekuwa ikitekeleza mradi wa ujenzi wa reli wenye thamani ya dola bilioni 3.1tango mnamo 2017.

Mradi huo wa reli utakapokamilika, utaunganisha Tanzania na Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mehmet Gulluoglu, balozi mkazi wa Uturuki, alisema kuwa nchi hizo zina matarajio ya mafanikio makubwa kutokana na uhusiano uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Tayari, Tanzania kupitia chama cha TCCIA imeanzisha Ofisi ya Diaspora kwa wafanyabiashara jijini Istanbul Uturuki, huku ikiunganisha Tanzania na soko la Kituruki.

TRT Afrika