Mamlaka ya KRA inalenga kuongeza kuokota mapato nchini mwaka huu / Picha: Reuters

Mjadala nchini Kenya kuhusu ni nini kinafaa kutozwa ushuru wa forodha ulianza wakati mamlaka ya mapato nchini Kenya, Kenya Revenue Authority, ilipoweka matangazo kwa mtandao wa kijamii kuashiria kuwa yeyote ataingia nchini na bidhaa yenye thamani ya dola 500 au zaidi atatozwa ushuru.

Tangazo hili ambalo KRA baadaye iliondoa , iliashiria kuwa yatakayotozwa ushuru ni hata bidhaa za watu binafsi.

" Niliona ni njia mzuri kwa sababu hiyo ni njia moja ya kuinua uchumi ya nchi na angalau hao watu ambao wanakuja nchini ," Mkaazi wa mji wa Nairobi ameambia TRt Afrika.

" Haifai, hivyo ni vitu vyangu hazistahili kwa ushuru wowote, watoze ushuru vitu vingine kama dawa au vitu vingine vya mauzo ya nje kama kahawa na chai lakini vitu vyangu hapana. Hiyo ni pesa yangu binafsi na visitozwe ushuru," mwananchi mwengien ameiambia TRT Afrika.

Mamlaka ya KRA baadaye ikanyoosha maelezo.

"Unaporudi nchini utarudi na nguo , mifuko uliyoenda nayo ," David Ontweka Afisa wa KRA ameelezea, " lakini ikiwa umenunua bidhaa za thamani ya dola 500 zaidi ya moja basi unahitajiwa kutambulisha zingine kwa ajili ya ushuru."

Lakini sheria inasemaje?

"Sio sheria ya kunyanyasa kwa sababu hii ndiyo sheria imekuwepo nadhani," Joseph Mwaniki, mtaalamu wa ushuru anaambia TRT Afrika.

" Mada ya majadiliano inapaswa kuwa ikiwa thamani ya kutozwa ushuru ipo katika viwango vinavyohitajika au inahitajika kuangaliwa tena iwe ya juu labda hata dola 1000 au kiwango chochote." Mwaniki amesema.

Kenya inatumia sheria ya ushuru wa forodha ya Afrika Mashariki 2004.

Sheria hii inahusisha:

  • Bidhaa za mtu binafsi zinazototumika au zilizotumika hazitozwi ushuru
  • Bidhaa zenye thamani ya $500 kwa kila msafiri haziruhusiwi kutozwa ushuru
  • Upukuzi wa migizo hufanywa kukagua bidhaa zilizopigwa marufuku na zilizozuiliwa kwa usalama wa nchi.
  • Mizigo ambayo itawekewa alama italazimika kugakuliwa tena na afisa wa KRA na abiria kuwasilisha mwenyewe mizigo inayofaa kutozwa ushuru.
  • Ushuru utakaolipwa (ikiwa upo) utatokana na bei halisi ya ununuzi kama ilivyowasilishwa na abiria/msafiri mwenyewe.

Mamlaka ya KRA ina lengo la kukusanya zaidi ya dola bilioni 13 katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Rais wa Kenya William Ruto ameambia mamlaka hii ya KRA iwache kutoza wananchi ushuru bila kuwanyanyasa.

TRT Afrika