Wanasoka wa Kiafrika waliotamba barani Ulaya msimu huu.

Wanasoka wa Kiafrika waliotamba barani Ulaya msimu huu.

Kuna Waafrika wengi wanaocheza katika vilabu mbalimbali vya kandanda barani Ulaya.
Achraf Hakimi, Hakim Ziyech - Picha/Reuters

Msimu wa mpira barani ulaya umekuwa wa kusisimua na ni wakati mwafaka wa kuangalia michango ya hali ya juu ya wanasoka wa Kiafrika.

Iwe kule Uhispania, Uingereza, Italia, Ufaransa au Ujerumani, nyota wa soka kutoka Africa kwa mara nyingine tena wameng'ara uwanjani na kufanya vyema wakiwa na klabu zao.

RIYAD MAHREZ

Mahrez ni mchezaji wa Manchester City. Michuano ya ligi ya Uingereza imemalizika kwa Manchester City kutwaa taji hilo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria, ambaye alifunga mabao 10 na kutoa pasi zilizopelekea City kufunga mabao kumi katika mechi zote, alichangia pakubwa katika ushindi wa timu yake.

Riyad Mahrez /Picha:Reuters

Baada ya kuwasili katika klabu hiyo mwaka wa 2018, Riyad Mahrez alishinda taji lake la nne la ligi akiwa na City na la tano nchini Uingereza. Alikuwa ameshinda ligi mwaka 2016 akiwa na Leicester.

VICTOR OSIMHEN

Napoli walitwaa taji lao la tatu la ligi ya Italia, zaidi ya miaka 30 baada ya kushinda mataji mawili ya awali wakati wa Diego Armando Maradona (1987 na 1990).

Victor Osemehen kutoka Nigeria Picha,

Kurejea kwa klabu hiyo ya Italia kwenye ligi kuu kulichochewa na wachezaji wengi wenye vipaji, akiwemo Victor Osimhen, nyota wa kimataifa wa Nigeria.

Osimhen alikabiliana na kila kikwazo katika njia yake. Mshambulizi huyo stadi aliisaidia klabu yake, akifunga mabao 31, yakiwemo 26 kwenye ligi - na kumfanya kuwa mfungaji bora wa Serie A mbele ya Lautaro Martinez aliyefunga mabao 21.

Mshambulizi huyo mzaliwa wa Lagos pia alitumia fursa ya msimu huu kuonyesha kipaji chake tena na kuwa mfungaji bora wa Afrika katika historia ya Serie A akiwa na mabao 50, kabla ya kuvunja rekodi ya wababe wengine wa Kiafrika George Weah na Samuel Eto'o wakati wa uchezaji wao.

FRANCK KESSIE

Baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, FC Barcelona walipata faraja katika La Liga na kushinda taji lao la kwanza chini ya mkufunzi Xavi Hernandez.

Franck Kessie mchezaji wa Barcelona

Kiungo huyo wa kimataifa wa Côte d'Ivoire alijiunga na Barcelona kutoka AC Milan na alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa timu yake. Alicheza jumla ya michezo 50 katika mashindano yote, akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu murua zilizopelekea Barcelona kufunga mabao.

SADIO MANE

Ubingwa ambao haukutarajiwa sana kwa Bayern Munich katika ligi ya ujerumani, Bundesliga, ulitokana na juhudi za Mane.

Miamba hao wa Bavaria walikuwa katika hali mbaya kuelekea siku ya mwisho ya ligi hiyo, wakilazimika kushinda katika jiji la Cologne na kutumai kwamba wapinzani wao Dortmund wangeteleza, na waliteleza.

Sadio Mane  /Picha/Reuters

Katika msimu wake wa kwanza nchini Ujerumani, Sadio Mané alishinda taji hilo baada ya msimu wa misukosuko kwa nyota huyo wa Senegal kutokana na vita vyake na mchezaji mwenza Leroy Sané, na kusababisha kusimamishwa na kupigwa faini.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na jeraha lililomfanya asishiriki michuano ya Kombe la Dunia, alifunga mabao 13 katika michezo 39 na kutoa pasi saba za mabao.

CHOUPO-MOTING NA NOUSSAIR MAZRAOUI

Noussair Mazraoui ni mchezaji wa kulipwa ambaye anacheza kama beki wa pembeni, kiungo wa kati au winga wa klabu ya Bundesliga ya Bayern Munich.

Baada ya kuwasili kutoka Ajax, raia huyo wa Morocco alicheza mechi 28 katika msimu wake wa kwanza akiwa na rangi za Bavaria, akifunga bao moja na kutoa pasi nne zlilizopelekea Bayern kufunga mabao.

Mazraoui Na Chopo-moting 

Hii ni sawa na kisa cha Éric Maxime Choupo-Moting wa Cameroon ambaye aliisaidia timu yake, Bayern Munic, kutwaa taji hilo kwa kufunga mabao 17 na kutoa pasi nne za mabao katika mechi 30 za michuano yote.

ACHRAF AKIMI

Akimi ni Raia wa Moroko ambaye alijiunga na klabu ya PSG mwaka wa 2021.

PSG ilimaliza msimu wa 2022-2023 kwa kushindwa kwa mabao 2-3 nyumbani na Clermont japo walitawazwa kuwa mabingwa wa Ufaransa.

Ashraf Hakimi /Picha/Reuters

Baada ya kufurahia Kombe la Dunia lenye mafanikio akiwa na Morocco, mchezaji huyo, beki wa kulia alicheza mechi 45, akifunga mabao matano na kutoa pasi zilizopelekea PSG kufunga mabao sita.

SACHA BOEY

Katika Supa Lig ya Uturuki, Galatasaray, ilishinda taji kwa mchango mkubwa wa mkameruni Sacha Boey. Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 alicheza mechi 38, akifunga bao moja na kutoa pasi nne zilizopelekea Galatasaray kufunga bao.

Super Lig - Galatasaray v Trabzonspor

Ingawa hajacheza sana msimu huu, Bouna Sarr wa Senegal (mechi 1 pekee iliyochezwa) yuko kwenye orodha ya mabingwa pia.

TRT Afrika