Türkiye yashinda taji kwenye Mashindano ya Dunia ya soka kwa wachezaji wasio na miguu yote miwili

Türkiye yashinda taji kwenye Mashindano ya Dunia ya soka kwa wachezaji wasio na miguu yote miwili

Türkiye ilinyuka Angola magoli 4-1 kwenye fainali ya mashindano hayo Jijini Istanbul.
ampute

Türkiye has won the 2022 Amputee Football World Cup, beating reigning champions Angola 4-1 in the final in Istanbul. Türkiye imetwaa taji la mashindano ya dunia ya soka kwa wachezaji wasio na miguu yote miwili , baada ya kuwapiga mabingwa watetezi Angola magoli 4 kwa 1.

Wenyeji Türkiye walionesha ushindani mkubwa hasa katika kipindi cha pili baada ya kuishi sare ya moja kwa moja katika kipindi cha kwanza. Goli la kwanza la wenyeji lilifungwa na Omer Guleryuz kabala ya Adao kutoka Angola kusawazisha. Rahmi Ozcan alifungia Türkiye la pili kupitia mkwaju wa penati kabla ya kufunga linguine la tatu; naye Serkan Dereli akakamilisha hesabu kwa kufunga la nne.

Rais wa Türkiye Recep Tayyip Erdogan alikuwa uwanjani kushuhudia vijana wake wakicheza. “Nawapongeza sana kwa kushinda na kuonesha ukakamavu kipindi chote cha mashindano.” Aliandika Rais Erdogan kwenye ukurasa wake wa twitter.

Timu hiyo ilifuzu hatua ya fainali siku ya Ijumaa baada ya kuilaza Uzbekistan goli moja kwa bila. Goli hilo la pekee lilitiwa kimiyani na Omer Guleryuz. Ikumbukwe Turkiye ilimaliza ya pili kwenye mashindano ya mwaka 2018 nchini Mexico nyuma ya Angola. Angola ‘waliwachachafya’ Türkiye magoli 5 kwa 4 kwenye fainali wakati huo.

AA