Mambo saba yaliyo na mvuti mkubwa katika dimba la dunia Qatar 2022

Mashabiki wa mpira wana matarajio makubwa kutoka kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2022 FIFA litakaloandaliwa Qatar. Ratiba yake ni baina ya tarehe 20 Novemba hadi 18 Disemba 18, itakua mara ya kwanza kombe la dunia kufanyika katika milki za waarabu.

Usikose hivi vigezo saba kuhusu kombe la dunia mwaka huu:

Messi aaga kombe la dunia

Kitengo cha Outlet Star+ cha Agentina kimemuhoji nyota wa soka Lionel Messi, amesadikisha kwamba dimba la kombe la dunia Qatar itakua mara ya mwisho kushiriki: “Je, ni dimba langu la mwisho kushiriki? Ndio, bila shaka, bila shaka.”

“Nahesabu siku chache kufikia dimba la kombe la dunia. Kidogo kuna wasiwasi vilevile. Nikitaraji iwe sasa hivi na wasiwasi uliokuwepo tiyari, ni kipi kitatokea,” Alitamka

“Kwa upande mmoja, tuna hamu ya kushiriki na upande mwengine, tunahofia kwamba itakwenda vizuri.” aliongezea kauli.

Anatajwa kuwa mchezaji bora wa soka, Messi, ana miaka 35, ataendelea kuchezea klabu ya Paris St Gerrmain mpaka huni 2023, kwa mtazamio wa kuongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja zaidi. Kwa kua alichezea klabu ya Barcelona hapo awali, alisema anawazia kua mkurugenzi wa spoti wa timu.

“Ningependa kua mkurugenzi wa spoti. Sijui iwapo itakua Barcelona or la, ama iwapo nitapata wajibu mwengine. Ila kama kuna uwezekano, ningepata kusaidia klabu hiyo,” Aliongezea.

Qatar imepata vyumba zaidi vya malazi kwa wasafiri, imezidisha muda wa metro

Bloomberg inaripoti kwamba maelfu ya vyumba hotelini na majengo ya Arbnb yaliyokua yamehifadhiwa kwa ajili ya timu za soka, sponsa na tiketi za mapema za wageni sasa zinapatikana kwa ajili ya umma, ilivyotangazwa awali.

Kulingana na msemaji wa Qatar, nchi “ipo tayari kupatia malzi kwa watu 130,000 kwa ajili ya dimba, na pia zaidi ya vyumba 117,000 viinapatikana.”

Nakala hiyo inaorodhesha upagazi kama njia mbadala kama ‘vyumba makhususi, mahema, vyumba vya Airbnb na meli za kujivinjari zenye vyumba 4,000.”

Watalii wanaohudhuria kombe la dunia kutoka kwa nchi jirani watapata ndege za kuingia na kutoka siku hiyo moja, na kuongezeka kwa idadi ya ndege kutoka nchi jirani kwa ushirikiano mwema wa mataifa.

Habari za Doha pia zinaripoti kwamba “Reli ya Qatar itasambaza treni 110 na kuongeza masaa ya kazi hadi masaa 21 ili kumudu kuongezeka kwa idadi ya watu wakati wa kombe la dunia.”

Glastonbury spider kushiriki

Habari za Doha, wakinukuu The Sun, waliandika kwamba waandaaji wa kombe la dunia la FIFA wamesajili Arcadia, wamiliki wa tamasha la Glastobury, ili kutumbuiza hadhira wakati wa kombe la dunia.

Tamasha la muziki, litakalo shirikisha wacheza santuri maarufu duniani na maonyesho ya mataa, wanatarajiwa kufanikisha onyesho hilo. The Sun inaripoti kwamba “tamasha la Arcadia’, pamoja na onyesho kuu la tani 50 la Glastonbury spider, inatoa nafasi ya takriban 15,000 kwa siku.”

Onyesho la jezi ya Maradona

Makavazi ya 3-2-1 Qatar Olympic and Sports imeandaa maonyesho mapya kwa kombe la dunia la FIFA. iliita ‘dunia ya soka’.

Tovuti ya makavazi inasema kwamba “wageni wataweza kuhuisha kumbukumbu bora za kombe la dunia, kupata kujua mchakato wa Qatar kupata kuandaa kombe la dunia na kuonyesha rwaza zake kwa dunia.”

Moja kati ya vitu adhimu kwenye maonyesho ni jezi ya kwanza mwanasoka wa Agentina Diego Maradona alipofunga bao mashuhuri linalotambulika kama ‘Mkono wa dhahabu’ mnamo mwaka 1986 dhidi ya Uingereza. Kulingana na habari za Doha,“Makavazi hayo yameomba jezi hiyo ya buluu, iliyouzwa mnadani Mai kwa kima cha dolaa milioni 9.3”

Sohail na Soraya, Panda ‘mabalozi’ wa uchina katika kombe la dunia

Uchina umetangaza Septemba 26, 2022 kwamba itatuma panda wawili, Sohail na Soraya, huko Doha Oktoba kablla ya kombe la dunia.

Kulingana na habari za Doha, “Licha ya kutoshiriki katika kombe la dunia, makampuni ya uchina yamechangia pakubwa katika ukuaji wa miradi nasibishi.”

Panda hawa ni kati ya ishara ya ‘nguvu nyepesi’ kidiplomasia, kuonyesha usuhuba na marafiki zake.

Itikadi, makala ya habari, yanatoa kumbukumbu ya utawala jadi wa mfalme wa kike Wu aliyetuma panda Japan katika karne ya saba, na kuhuishwa nyakati za utawala wa Mao Zedong.

Wimbo wa kiarabu ‘Arhbo’ umevuma

Wimbo ‘Arhbo’ uliozinduliwa katika warsha ya kombe la dunia la FIFA mwanzo wa September umejizolea takriban wasikilizaji milioni 16 katika Youtube.

Wimbo unaelezwa na habari za Doha kua ‘mgando wa ndimi za waarabu wengi kwa mtindo wake wa mnato… ulipata kukubaliwa pindi tu ulipozinduliwa.”

Ripoti kutoka habari za Doha unasema video ya muziki ulisimamiwa na vipaji vya Qatar Mohamed al Ibrahim na kutayarishwa na Katara Studios Doha.

Uliimbwa na wanamuziki kutoka miliki ya ghuba, na kanda hiyo inahusisha Nasser al Kubaisi, mwanamuziki mchnaga qatar, mwanamuziki wa Saudia na mwanamuziki Ayed Yousef ambae alikua moja wapo wa majaji wa shindano la kwanza Saudia la uimbaji ‘Nishinde iwapo unaweza.’ na Haneen Hussein, alinakili wimbo maarufu wa ‘Bravo Alek’ pamoja na Abdelaziz Lewis na Bdr al Shuaibi ambayo ilitizamwa na zaidi ya mara milioni 117 katika Youtube.

Qatar Philharmonic kuhudhuria warsha la ufunguzi

Ukizuru Doha katika kombe la dunia la FIFA, kuna uwezo kwamba utakumbana na oketsra ya Qatar Philharmonic ikitumbuiza nje kwa ustadi. Badala ya utumbuizaji wa nakshi, QPO itaonyesha “viwanja mashuhuri duniani, nyimbo za kiarabu, midundo ya kiarabu, na vibao vilivyoundwa na okestra ya Philharmonic” kilingana na Mkurugenzi mwendeshaji, Kurt Meister, aliyeambia Shirika la habari la Doha kwamba matamasha nane hadi kumi yatafanyika hadharani.

“Tumeweka mikakati kuwepo na nyimbo mashuhuri za soka kutoka nchi tofaut tofauti.”

TRT World