Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2024, Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), limethibitisha.
Nchi hiyo ilikuwa ikiwania nafasi hiyo adimu peke yake, huku uthibitisho wake ukiwekwa wazi siku ya Jumatano katika kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao, kikihusisha wanachama 211 wa FIFA.
Saudi Arabia inakuwa nchi ya pili kutoka eneo la Mashariki ya Kati, kuandaa michuano hiyo mikubwa ulimwenguni, baada ya Qatar kufanya hivyo mwaka 2022.
Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika katika viwanja 15 katika miji ya Riyadh, Jeddah, Khobar, Abha, na Neom ndani ya himaya ya ufalme wa Saudi Arabia.
Katika hatua nyingine, FIFA imezitangaza Ureno na Hispania kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2030, huku Morocco ikipata bahati kuandaa michuano hiyo kwa upande wa bara la Afrika, wakati Uruguay, Paraguay na Argentina zitapata nafasi ya kuandaa michezo ya kwanza, ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 100 ya michuano hiyo mikubwa duniani.
Kulingana na FIFA, michuano ya Kombe la Dunia kwa 2026, itaandaliwa na mataifa ya Mexico na Canada.