Saint-Germain ilibainisha tu kwamba anasalia chini ya mkataba hadi Juni 30 / Photo: AFP

Mapema leo iliripotiwa kuwa Nyota wa Argentina Lionel Messi atacheza nchini Saudi Arabia msimu ujao chini ya mkataba "mkubwa", chanzo chenye ujuzi wa mazungumzo hayo kilisema.

"Messi yuko tayari. Atacheza Saudi Arabia msimu ujao," kilisema chanzo Jumanne, kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina na bila kutaja klabu hiyo. "Mkataba ni wa kipekee. Ni mkubwa. Tunakamilisha mambo madogo," chanzo hicho kiliongeza.

Ilipoulizwa kuhusu maoni hayo, klabu ya sasa ya Messi ya Paris Saint-Germain ilibainisha tu kwamba anasalia chini ya mkataba hadi Juni 30.

Baba mzazi wa Messi akanusha

Hata hivyo bila kuchelewa, Babake Messi, Jorge, alitoa taarifa ya kukanusha baada ya ripoti za mapema siku hiyo kusema kwamba fowadi huyo atasaini mkataba mkubwa wenye thamani ya pauni milioni 522 katika klabu ya Al-Hilal ya Saudia.

"Hakuna chochote na klabu yoyote kwa mwaka ujao. Uamuzi huo hautawahi kufanywa kabla ya Lionel kumaliza ligi akiwa na PSG".

'Msimu ukiisha itakuwa ni wakati wa kuchambua na kuona kuna nini, na kisha kufanya uamuzi, aliongeza baba wa Messi.

Pia alishutumu walio paisha taarifa hiyo kama wanalengo la kunufaika tu kwa kupitia jina la mtoto wake. Huku akisisitiza hakuna mkataba wowote ulio sainiwa au kukubaliwa.

"Siku zote kuna uvumi na wengi hutumia jina la Lionel kupata sifa lakini ukweli ni mmoja tu na tunaweza kuhakikisha kuwa hakuna kitu na mtu yeyote. Wala kwa maneno, wala kusainiwa, wala kukubaliwa, na hakutakuwa na hadi mwisho wa msimu".

Endapo Messi atakwenda katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta itakua amefuata nyayo za Cristiano Ronaldo, ambaye alijiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Pro League kwa mkataba mkubwa mwezi Januari

AFP