Ujerumani ndio mabingwa Kombe la Dunia U-17, Indonesia 2023

Ujerumani ndio mabingwa Kombe la Dunia U-17, Indonesia 2023

Ujerumani ilitwaa Kombe hilo la U-17 kupitia mikwaju ya penalti dhidi ya Ufaransa
#LCJ53 : FIFA U-17 World Cup / Photo: AFP

Ujerumani imeipiga Ufaransa kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti na kutwaa Kombe La Dunia kwa wanasoka wasiozidi miaka 17 nchini Indonesia siku ya Jumamosi, na kuwa timu ya kwanza kushinda mataji ya umri huo duniani na Ulaya ndani ya mwaka huo huo.

Mchuano huo ulienda hadi muda wa ziada baada ya timu hizo kukabana 2-2 katika hali ya unyevu huko Surakarta, kisiwa cha Java.

Wajerumani hao chipukizi kisha walishikilia ujasiri wao kipindi cha penalti na kufanikiwa kuwapiga Blues na kushinda taji lao la kwanza la Ulimwengu chini ya miaka 17 iliyokuwa ni kama mechi ya marudiano ya fainali ya mashindano ya Ulaya ya mwaka huu, ambayo pia walishinda kupitia mikwaju ya penalti.

Mlindalango Konstantin Heide alikuwa shujaa wa Ujerumani kwa mara nyingine, huku akiokoa penalti mbili kabla ya nyota wa Borussia Dortmund Almoguera Kabar kufunga bao la ushindi na kukamilisha ushindi kwenye mikwaju 4-3.

Nyota wa Ujerumani Paris Brunner alitawazwa mchezaji bora wa mashindano hayo baada ya mfululizo wa maonyesho ya kipekee na kufunga mabao matano kwenye mashindano hayo. Picha: AFP

Pande zote, Ujerumani na Ufaransa zilipoteza penalti mbili kila moja huku na kufufufa matumaini ya wapinzani wao kwenye mikwaji kabla ya Tidiam Gomis kukosa shuti ya mwisho.

Ujerumani ilikuwa kifua mbele kwa mabao mawili katika muda wa kawaida, kupitia mshambuliaji hodari wa Borussia Dortmund Paris Brunner katika dakika ya 28 na nahodha Noah Darvich katika dakika ya 50, lakini kikosi cha Ufaransa chenye juhudi nyingi kilisawazisha.

Ufaransa ilijibu kupitia Salmon Bouabre wa Monaco, Mathis Amougou katika dakika ya 85.

Ufaransa iliwazidi Ujerumani kwa mchezaji mmoja baada ya mchezaji wa Ujerumani Osawe kulishwa kadi nyekundu kwa kumwumiza Ismail Bouneb kwani tayari alikuwa amelishwa kadi ya manjano.

Hata hivyo, Ulinzi thabiti wa Ujerumani kisha ulishikilia hadi hatua ya penalti ambayo ingewapa taji, na kufanikiwa kuwa mabingwa wa 2023.

Aidha, bara la Afrika pia limenawiri kwenye kombe hilo baada ya Mali kupokea medali ya shaba kwa kumaliza katika nafasi ya tatu.

Pia, kiungo Hamadou Makalou ametunukiwa mchezaji bora wa pili kwenye fainali hizo kwa kuonyesha fomu nzuri kwa upande wa Mali kwenye fainali hizo za U-17, na kucheza vyema kwenye fainali hizo.

Nahodha wa Mali Ibrahim Diarra alipewa kiatu cha fedha kwa kuwa mfano bora kwenye fainali za U17. Diarra alihusika katika mabao 9 kati ya 18 yaliyofungwa na timu yake kwenye mashindano hayo, na alikuwa wa kuvutia sana katika ushindi wao wa robo fainali dhidi ya Morocco na mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Argentina.

TRT Afrika na mashirika ya habari