Kombe la Dunia la Raga 2023: Waathiriwa wa majanga Libya na Morocco Kukumbukwa uwanjani

Kombe la Dunia la Raga 2023: Waathiriwa wa majanga Libya na Morocco Kukumbukwa uwanjani

Wakati wa mshikamano utazingatiwa mbele ya nyimbo kwenye mechi ya Kombe la Dunia la Raga kati ya Ufaransa na Uruguay 2023
Kombe la Dunia la Raga/ Picha: AFP

Mchuano wa Kundi A kati ya Ufaransa na Uruguay utakaochezwa huko Lille, Ufaransa Alhamisi utawakumbuka wale walioathiriwa na mafuriko nchini Libya na tetemeko la Ardhi Moroko.

Timu zote zinazoshiriki Kombe la Dunia la Raga 2023 na jumuiya nzima ya raga ulimwenguni zinaalikwa kujiunga na kipindi cha mshikamano Kombe la dunia la Raga 2023 na familia ya raga ulimwenguni inasimama kwa mshikamano na watu wa Libya na Morocco katika wakati huu mgumu sana.

Kombe la dunia la Raga

Kombe la dunia la Raga Duniani nchini Ufaransa 2023 imethibitisha kwa taarfia awali kuwa muda wa mshikamano na dakika la kimya litazingatiwa kabla ya nyimbo za taifa Katika mechi kati ya Ufaransa na Uruguay.

"Muda wa mshikamano utafanywa kuwakumbuka wale ambao wamepoteza maisha yao, wapendwa waliopotea, na wote walioathiriwa na mafuriko nchini Libya na tetemeko la ardhi nchini Morocco." Kombe la Dunia la Raga lilisema.

TRT Afrika