Mali sasa itacheza dhidi ya Argentina kuwania nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia la Vijana chini ya miaka 17. / Picha: TRT Afrika

Wajerumani waliishinda Argentina 4-3 katika mikwaju ya penalti kufuatia sare ya 3-3 siku ya Jumanne. Ufaransa iliishinda Mali 2-1.

Paris Brunner aliifungia Ufaransa mabao mawili naye Max Moerstedt akaongeza jingine mjini Surakarta.

Fowadi wa Argentina Agustine Roberto aliifungia timu yake mabao matatu ‘hat trick’ na kufikisha mabao nane katika michuano hiyo ya mataifa 24.

Yvann Titi na Ismail Bouneb walifunga bao kila mmoja kwa Ufaransa, ambayo ilishinda taji la U17 mnamo 2001. Ibrahim Diarra aliifungia Mali.

Fainali ya Jumamosi itachezwa huko Surakarta. Argentina na Mali zitakutana katika jiji moja siku moja mapema katika mchujo wa kuwania nafasi ya tatu.

TRT Afrika