CAF : Kinyang'anyiro cha kocha bingwa wa mwaka  Afrika

CAF : Kinyang'anyiro cha kocha bingwa wa mwaka  Afrika

Walid Al-Raghraghi, Aliou Cisse, na Abdelhak Ben Sheikha ndio watatu walioangaziwa.
Makocha hao watatu wameziongoza timu zao kwa ubora wa soka. Picha: CAF

Sherehe za Tuzo za CAF 2023 zimepangwa kufanyika Jumatatu, Desemba 11, 2023, huko Marrakech, Morocco, na hadi sasa kil ammoja anabahatisha ni nani atatwaa tuzo kuu za CAF za Wachezaji Bora wa Mwaka.

Hata hivyo, ingawa kuna uangalizi mkubwa kwa wachezaji watatu bora walioteuliwa katika kitengo cha wanaume (Mohamed Salah, Achraf Hakimi, na Victor Osimhen) na kitengo cha wanawake (Asisat Oshoala, Thembi Kgatlana, na Barbara Banda), hebu tuangalie walio juu upande wa makocha watatu wa Kiafrika (timu za kiume) walioteuliwa kuwania tuzo hizo mwaka huu.

Walid Al-Raghraghi, Aliou Cisse, na Abdelhak Ben Sheikha ndio watatu walioangaziwa, na mshindi atatangazwa katika sherehe za zilizoandaliwa za kutolewa tuzo siku ya Jumatatu.

Walid Regragui (Morocco)

Walid Al-Raghraghi aliiongoza Morocco kufika kilele kisichofikiriwa katika Kombe la Dunia la Qatar alipowafikisha nusu fainali ya kwanza kabisa ya Afrika katika fainali za Kombe la Dunia la FIFA, huku Morocco ikishika nafasi ya 4.

Walid Al-Raghraghi aliiongoza Morocco hadi nafasi ya 4 katika Kombe la Dunia la Qatar. Picha: Nyingine

Pia amepata mafanikio makubwa katika ngazi ya klabu, huku Wydad AC ikifika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa CAF na Ligi ya Soka ya Afrika.

Aliou Cisse (Senegal)

Cisse ndiye kocha bora wa sasa wa mwaka wa CAF na atakuwa na matumaini ya kuhifadhi tuzo hiyo baada ya kazi yake nzuri akiwa na timu ya taifa ya Senegal, ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika.

Cisse ndiye bingwa metetzi wa cheo hicho kikubwa zaidi cha makocha Afrika : Picha: AFP

Cisse pia aliiongoza Simba wa Teranga kutinga Raundi ya 16 ya Kombe la Dunia la FIFA la Qatar kabla ya kuondoka kwenye michuano hiyo baada ya kushindwa na Uingereza.

Abdelhak Benchika (Algeria)

Ben Sheikha anatambulika kwa kazi yake na USM Algiers. Picha: AFP

Abdelhak Ben Sheikha alikuwa na msimu mzuri na USM Alger msimu uliopita, huku wakishinda taji lao la kwanza kabisa la Kombe la Shirikisho la CAF.

Hili lilifuatiwa na kunyanyua tena kwa kihistoria kwa CAF Super Cup baada ya kuwashinda wababe wa Misri Al Ahly.

Ingawa Sheikha kwa sasa amejiunga na wababe wa Tanzania, Simba AC, kazi yake imemfanya aingie kwenye kinyang'anyiro cha kuwania taji hilo.

TRT Afrika