Ballon d’Or 2023: FIFA yatangaza wachezaji 12 watakaopigiwa Kura kuwania Mwanasoka Bora duniani

Ballon d’Or 2023: FIFA yatangaza wachezaji 12 watakaopigiwa Kura kuwania Mwanasoka Bora duniani

Lionel Messi, Victor Osimhen, Erling Haaland, Kylian Mbappé, Declan Rice, na Kevin De Bruyne, miongoni mwa mastaa 12 watakaopigiwa kura.
Tuzo za FIFA za Mchezaji Bora wa Dunia 2023 zitatolewa katika sherehe ya Ballon D'or, ambayo itafanyika Oktoba 30, Ufaransa. Picha: FIFA

Mchezaji bora wa kiume na kike, Kocha bora wa timu ya wanaume, Kocha bora wa timu ya wanawake, kipa Bora wa wanaume, na kipa bora wa wanawake watapigiwa kura.

Mashabiki wa Soka kote ulimwenguni wameanza kupiga kura kuwachagua wanasoka bora duniani 2023 katika vitengo kadhaa huku FIFA ikitarajiwa kuwatawaza rasmi mastaa wa soka la wanawake na wanaume mwaka huu.

FIFA imetoa orodha ya washindani 12 watakaopigiwa kura na mashabiki huku kila mmoja wa mastaa hao wakitambuliwa kwa ubora wao endelevu na michango yao mpirani katika kipindi hicho kati ya tarehe 19 Desemba 2022 hadi 20 Agosti 2023.

Kwa kitengo cha mchezaji bora wa kiume, Julian Alvarez, Marcelo Brozovic, Kevin De Bruyne, Ilkay Gundogan, Erling Haaland, Rodri, Khvicha Kvaratskhelia, Kylian Mbappe, Lionel Messi, Victor Osimhen, Declan Rice na Bernardo Silva ndio wachezaji 12 watakaowania tuzo hiyo.

Kwa kitengo cha mwanasoka bora wa kike, tuzo hiyo itanyakuliwa na mmoja kati ya wachezaji walioteuliwa Aitana Bonmati, Linda Caicedo, Rachel Daly, Kadidiatou Diani, Caitlin Foord, Mary Fowler Alex Greenwood, Jennifer Hermoso, Lindsey Horan, Amanda Ilestedt, Lauren James, Sam Kerr, Mapi Leon, Hinata Miyazawa, Salma Paralluelo, na Keira Walsh.

Vitengo mbalimbali vitakavyopigiwa kura

  • Mchezaji Bora wa Wanawake wa FIFA
  • Mchezaji Bora wa Wanaume wa Fifa
  • Kocha Bora wa Wanawake wa FIFA
  • Kocha Bora wa Wanaume wa FIFA
  • Kipa Bora wa Kike wa FIFA
  • Kipa Bora wa Wanaume wa Fifa
  • Tuzo Ya Shabiki wa FIFA

Wachezaji wa Argentina na Manchester City wametawala orodha hiyo kufuatia ushindi wa Argentina wa Kombe la Dunia na ubingwa wa Manchester City wa Ligi ya Mabingwa Champions League, Ligi kuu ya Uingereza na mataji ya Kombe la FA, na UEFA Super Cup.

Lionel Messi analenga kujiongezea tuzo yake ya nane ya Ballon D'or baada ya kushinda mara saba hapo awali huku akitarajiwa kupigiwa kura kutokana na mchango wake kwa soka mwaka huu.

Nahodha huyo wa Argentina aliiongoza nchi yake kutwaa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, na kuisaidia klabu yake ya awali ya PSG, kushinda taji la Ligue 1 nchini Ufaransa.

Hata hivyo, nyota huyo, Messi, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mashine ya magoli Erling Haaland wa Manchester City ambaye analenga kushinda tuzo hiyo ya kifahari kwa mara yake ya kwanza.

Mashine ya magoli, Erling Haaland ndiye mshindani mkuu dhidi ya Messi. Picha: UEFA
Aidha, nyota wa kiume wa Afrika wanaosubiri kura za mashabiki ni pamoja na staa wa Misri, Mohamed Salah anacheza soka ya kulipwa Liverpool, André Onana wa Cameroon aliyecheza Inter awali kabla ya kuhamia Manchester United, Victor Osimhen - wa Napoli na timu ya taifa ya Nigeria, na Yassine Bounou - Sevilla-Al Hilal/Morocco.

Tuzo ya kipa bora wa wanaume wa FIFA zitawaniwa na Yassine Bounou, Thibaut Courtois, Ederson, Andre Onana, na Marc-Andre ter Stegen.

Mackenzie Arnold, Ann-Katrin Berger, Catalina Coll, Mary Earps, Christiane Endler, Zecira Musovic na Sandra Panos Garcia-Villamil watawania tuzo ya kipa bora wa wanawake.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola atagombe kocha bora wa timu za wanume dhidi ya Simone Inzaghi, Ange Postecoglou, Luciano Spalletti na Xavi kwa kitengo cha bora .

Kwa upande wa kocha bora wa timu za kike, Peter Gerhardsson atashindania taji hilo dhidi ya Jonatan Giraldez, Tony Gustavsson, Emma Hayes na Sarina Wiegman.

Kwa upande mwingine, Mchezaji Bora wa wanawake, Kocha Bora Wa Wanawake na Kipa Bora wa Wanawake kutambuliwa kwa michango yao kwa mchezo mzuri kati ya 1 agosti 2022 hadi 20 agosti 2023, tarehe ya Fainali Ya Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA.

Lionel Messi analenga kujiongezea tuzo yake ya nane ya Ballon D'or baada ya kushinda mara saba hapo awali huku upigaji kura kwa wachezaji bora duniani ukianza.

Washindi watatangazwa katika sherehe ya Ballon D'or ambayo itafanyika Oktoba 30 Katika Ukumbi wa Theatre du Chatelet huko Paris, Ufaransa.

TRT Afrika