Ushindi huo umefufua matumaini ya Ureno ya Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake na kuiwezesha Vietnam kutemwa kutoka mchakato huo wenye ushindani mkali.
Marefa Salima Mukansanga kutoka Rwanda na Mary Njoroge kutoka Kenya wameweka historia kwa kusimamia mechi ya Kombe la dunia la Kundi E kati ya Ureno na Vietnam uliopigwa uwanjani Waikato, mjini Hamilton, Australia.
Salima na Mary, wawakilishi pekee kutoka Afrika mashariki kati ya marefa 33 na manaibu 55 walioitwa miongoni, walijizolea sifa kwa usimamizi wao wa ngarambe hiyo.
Wawili hao walikuwa katika jumla ya mahakimu 106 waliotambulishwa kusimamia mechi za kombe la dunia la wanawake mwaka huu..
Mkenya Njoroge anashiriki kombe lake la pili la dunia baada ya kuwa naibu refa wa mechi ya Kombe la Dunia la wanawake 2019, na mechi za soka Olimpiki 2020 ambapo aliweza kuonyesha utaalamu wake.
Njoroge, mwenye umti wa miaka 38, aliwasili Australia juma lililopita kushika doria mechini kufuatia taarifa ya FIFA iliyomteua kwenye orodha ya marefa iliyomuarifu kuhusu uteuzi wake.
"Ninafurahia sana kazi hii yangu. Kwa kweli imekuwa miaka minne ya maandalizi ya hali ya juu, na ninafurahia kwamba umefika wakati wa kufanya ninachopenda zaidi.Udogoni mwangu, sijawahi kuwa na shauku ya mpira wa miguu.
“Siku moja nilipewa changamoto na mtu kusomea kozi ya waamuzi. Sikuwa na mtazamo mazuri kuhusu hilo kwa sababu nilihisi kuwa, waamuzi wana upendeleo. Hatimaye, nilichukua changamoto, na hali ilikuwa tofauti. Ilinichukua muda mwingi kujiandaa na kutambulika kwa kazi yangu," alihitimisha.
Mrwanda Salima Mukansanga, naye ameendelea na safari yake ya kuweka historia kwa kuwa refa mkuu wa mechi hiyo.
Mnamo 2019, Mukansanga, aliweka historia kwa kuwa mwamuzi wa kwanza wa kike wa kiafrika katika toleo hilo la Kombe la Dunia la Wanawake.
Refa huyo alipata umaarufu mwaka uliopita kwa kuwa refa wa kwanza wa kike wa kiafrika kuhudumu katika kombe la dunia la wanaume mwaka jana nchini Qatar. Kombe hilo lilikuwa la kwanza ambayo mechi imesimamiwa na waamuzi wa kike kwenye mashindano ya wanaume.
Aidha, mnamo mwaka jana, aliweka historia kwa kuwa hakimu mkuu wa kwanza wa kike kwenye ngarambe za Afcon kwa wanaume nchini Cameroon.
Mukansanga mwenye umri wa miaka 34, amehitimu na shahada ya kwanza ya Uuguzi na Ukunga kutoka Chuo Kikuu cha Gitwe, kilichoko Wilaya ya Ruhango, Mkoa wa Kusini wa Rwanda.