Wakati Kipchoge alipovuka safu ya kumaliza, Mshindi upande wa wanawake Tigst Assefa alikuwa dakika tatu mbele ya rekodi ya dunia ya 2:14:04.
Ushindi wa tano wa Kipchoge unamfanya ampiku aliyekuwa akishikilia rekodi hio, Muethiopia Haile Gebrselassie, aliyekuwa ameshinda marathon hiyo mara nne.
Assefa avunja rekodi
Tigst Assefa wa Ethiopia alivunja rekodi ya Dunia ya wanawake wa Marathon kwa kumaliza kwa muda wa saa 2, dakika 11, sekunde 53 kushinda tena Berlin Marathon Jumapili.
Assefa alishinda Berlin Marathon ya mwaka jana kwa saa 2:15:37, ambayo ilikuwa ya tatu kwa kasi zaidi kwa wanawake katika historia. Asefa mwenye umri wa miaka 29 alipunguza zaidi ya dakika mbili kutoka kwa rekodi ya awali ya saa 2:14.04 - iliyokuwa imewekwa na Mkenya Brigid Kosgei huko Chicago, Marekani, mwaka 2019.
Muda wake pekee wa mbio za marathon kabla ya hapo ulikuwa 2:34:01 (katika mbio ambazo alikimbia akiwa amejeruhiwa). Kabla ya hapo, alikimbia mbio za mita 800 na kuondolewa katika mbio za Olimpiki za Rio 2016.