Safari ya kuwasaka wawakilishi wa ukanda wa CECAFA kwa kombe la TotalEnergies Caf (AFCON) U-20, ukanda wa cecafa kuanza rasmi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kuanzia tarehe 6- hadi tarehe 20 Oktoba.
Timu za mataifa wanachama ambazo zimethibitisha kushiriki ni pamoja na; Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania na Uganda.
Aidha, viwanja vitatu vikiwemo Azam Complex, uwanja wa KMC, na ule wa Meja Jenerali Isamuhyo ambavyo viko Dar es Salaam, vitatumika kwa ngarambe hizo.
Mashindano hayo yatayofunguliwa kwa Mechi ya Kundi A kati ya Sudan na Djibouti Oktoba 6 kwenye Uwanja Wa Meja Gen Isamuhyo.
Aidha, Tanzania watakwaruzana na Kenya katika Mechi ya Pili ya Kundi A itakayochezwa pia ndani ya siku ya kwanza kwenye Uwanja huo wa Isamuhyo.
Mechi za makundi zitafikia kilele Oktoba 15, ambapo timu mbili bora kutoka kila kundi zitajinyakualia nafasi kwenye hatua ya nusu fainali, huku mechi hizo zikichezwa siku tatu baadaye.
Mabingwa wa Kombe hilo, watafuzu moja kwa moja kuwakilisha CECAFA kwenye mashindano ya AFCON U-20 yatakayofanyika mwaka ujao.
Kundi A: Tanzania, Sudan, Rwanda, Djibouti, Kenya
Kundi B: Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Ethiopia
TRT Afrika na mashirika ya habari