Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imefuzu Kombe la Mataifa bora Afrika kwa Wanawake, Morocco 2024 na kuwa mwakilishi pekee wa Afrika Mashariki.
Fomu bora ya mshambulizi wa klabu ya Besiktas ya Uturuki, Opah Clement, mchuano wa mkondo wa kwanza, iliiwezesha Twiga stars kuwa na guu moja ndani ya WAFCON 2024.
Ushindi wake wa mechi ya awali iliiwezesha Twiga stars kushinda kwa jumla ya 3-1 kwa kushinda mechi ya kwanza.
Mchuano wa ugenini dhidi ya Togo uliopigwa Stade de Kegue Lome, Togo, uliisha 1-0.
Kabla ya kufuzu kumenyana na Togo, Tanzania iliibuka na ushindi 5-3 dhidi ya Cote D'ivoire kwa njia za penalti baada ya pande hizo kutoka sare ya 2 2.
Ingawa ilikuwa ni safari ndefu, Tanzania hatimaye imekamilisha mbio hizo kwa kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika la Wanawake la, Morocco 2024.
Mara ya mwisho Twiga Stars kufuzu fainali za Afcon kwa wanawake ilikuwa ni 2010 ilipoifunga Ethiopia kwa jumla ya mabao 4-2.
Tanzania ilimaliza mbio hizo baada ya kupata nafasi Katika Kombe la Mataifa Ya Afrika La Wanawake La TotalEnergies Caf, Morocco 2024 ambalo lilimalizika wiki hii.