Kombe la Dunia chini ya miaka 20, Tunisia, Gambia waingia uwanjani

Kombe la Dunia chini ya miaka 20, Tunisia, Gambia waingia uwanjani

Afrika imeanza kwa kishindo baada ya Nigeria kunyakua ushindi wa mechi yao ya ufunguzi
Kombe la dunia la U 20 linaendelea kwa siku ya tatu huku Timu za Afrika zikianza vyema kwa ushindi wa Nigeria PICHA:AFP

Jumatatu Afrika inaweka matumaini yake kwa Tunisia katika mechi yao ya ufunguzi ya kombe la dunia la wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 dhidi ya England.

Tunisia watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya England ambao ni mabingwa wa kombe hilo 2017. Wamo katika nafasi ya tatu katika kundi lao C kulingana na alama za kufuzu, katika kundi moja na Uruguay na Iraq.

Gambia nao pia watamenyana uwanjani na Honduras katika uwanja wa Mendoza nje ya mji mkuu Buenos Aires. Gambia walipenya shindano hili kufuatia kufika fainali ya kombe la U-20, na kushika nafasi ya pili nyuma ya washindi Senegal.

Hii ni mara ya pili kwa Gambia kuwahi kufuzu shindano hili la kidunia la wachezaji chini ya miaka 20.

Kombe la Dunia la U 20 linaendelea nchini Argentina huku timu za Afrika zikionesha matumaini ya kusonga mbele : Picha AFP

Mataifa ya Afrika yamefunguliwa mechi zao katika kombe la dunia la wachezaji wasiozidi 20, kwa ushindi kutoka kwa timu ya Nigeria.

Flying Eagles, waliicharaza timu ya Dominican Republic 2-1 nchini Argentina na kufungua matumaini ya nchi hiyo kujitengenezea jina katika mchuano huo unaotazamiwa kuwa kivuli cha kombe la dunia.

Flying Eagles walianza kwa kuyumba baada ya Dominican Republic kutikisa wavu wao dakika 24 baada ya mechi kuanza.

Hata hivyo dakika nane baadaye mlinzi wa upande wa kushoto wa Dominican aliwatendea wenzake madhambi alipojifunga na kuwasawazishia Flying eagles na hivyo kuwainua hamasa zao.

Samson Lawal naye akaingia nusu ya pili kwa mikeke huku akiihakikishia timu yake ushindi kwa bao lake dakika ya 72. Sasa Nigeria itakutana na Italy katika mechi yao ya pili ya Kundi D

Timu ya Pekee Afrika U 2- iliyowahi kushinda kombe hili ni Ghana. Senegal walizana kampeni yao kwa kushindwa na Japan : Picha AFP

Kwa upande wake Senegal haikuanza vyema ambapo mechi yao ya kwanza walifungwa 1-0 na Japan.

Samurai hao walijinyakulia alama tatu za mechi hiyo kupitia Kuryu Matsuki ambaye tangu kuanza kwa mechi alionesha kuwa kitisho wa simba wadogo wa Teranga.

Hata hivyo juhudi za Simba hao kusawazisha ziligonga ukuta pale mkwaju mkali na bao la Souleymane Faye lilikataliwa kutokana na kuotea. Mechi ilimalizika bila bao lingine.

Sasa Senegal imewekeana miadi na Israel siku ya Jumatano katika mechi yao ya pili ya kundi C.

TRT Afrika