Marais wa mashirikisho ya soka barani Afrika na wasimamizi wa mchezo wamejumuika mjini Abidjan Côte d'Ivoire kujua hatma ya timu zao za taifa wakati droo ya awali ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026 itakapofanyika.
Kombe la Dunia, litaandaliwa kati ya Juni 11, na Julai 19, 2026 katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada, likiwa na timu 48.
Timu zote 54 wanachama wa Shirikisho la soka barani CAF, zimegawanywa kwa vyungu 9, mbele ya droo hiyo itakayofanyika Abidjan Côte d'Ivoire.
Droo itakapokamilika, kutakuwa na makundi 6 ya timu 9 kila kundi.
Muundo wa vyungu vya droo yaani ‘pots’ utakaotumika kukutanisha timu kutoka vyungu tofauti kama ilivyopangwa na shirikisho la soka Afrika
Chungu 1: Nigeria, Morocco, Senegal, Algeria, Tunisia, Cameroon, Mali, Misri
Chungu 2: Ghana, Burkina Faso, Afrika Kusini, Cape Verde, DR Congo, Guinea, Zambia, Gabon, Equatorial Guinea
Chungu 3: Angola, Benin, Kenya, Mauritania, Congo, Uganda, Madagascar, Guinea Bissau, Namibia
Chungu 4: Msumbiji, Gambia, Sierra Leone, Togo, Tanzania, Zimbabwe, Central African Republic, Malawi, Libya
Chungu 5: Niger, Comoros, Sudan, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eswatini, Botswana, Liberia
Chungu 6: Lesotho, South Sudan, Mauritius, Chad, Sao Tome, Djibouti, Seychelles, Eritrea, Somalia
Mshindi wa kila kundi atajihakikishia nafasi katika kombe la Dunia 2026.
Kombe la Dunia 2026 litakuwa na timu 48 baada ya kuongezwa kutoka timu 32 mnamo mwaka wa 2017.