Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamati ya Kitaifa ya Majadiliano, pande hizo zilitia saini masuala mbalimbali yakiwemo masuala ya kikatiba yasiyokamilishwa, haki ya uchaguzi na mambo yanayohusiana nayo, kuingiza fedha katika katiba, na uanzishwaji wa Ofisi za Nchi na uaminifu kwa vyama vya Siasa/Miungano na sheria ya demokrasia ya vyama vingi.
Uanzishaji wa ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na ofisi ya Mkuu wa mawaziri itajadaliwa chini ya mazungumzo ya uanzilishi na Uanzishwaji wa Ofisi za Nchi.
"Uaminifu, uwazi na uadilifu ndio msingi wa mazungumzo ya kweli na hilo ndilo tunalokuza hapa Bomas of Kenya na Viongozi wenzetu wa Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo wakiongozwa na Kimani Ichungwa." Alisema Kalonzo Musyoka.
Vile vile, ukarabati wa tume ya uchaguzi pia imetajwa kuwa miongoni mwa hoja maalum za mazungumzo ya kitaifa Kenya ikiwemo ukaguzi wa uchaguzi wa urais uliopita wa 2022.
Marekebisho na uundaji upya wa tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) pia imeshirikishwa kwenye mazungumzo ya pande hizo.
- Makubaliano ya Mfumo-kazi (makubaliano ya kuanzisha mfumo ulioundwa wa mazungumzo ya kitaifa na mazungumzo kuhusu masuala yanayohusiana na Taifa la Kenya)
- Taarifa ya masuala ya mazungumzo na kamati ya mazungumzo ya kitaifa (bila mpangilio maalum).
- Muda wa mazungumzo.
Masuala mengine muhimu yaliopewa kipaumbele ni pamoja na kujadili gharama ya Maisha na masuala yanayohusiana nayo, utekelezaji wa "kanuni ya kijinsia ya theluthi mbili", masuala ya utawala, ikiwa ni pamoja na kukuza umoja wa kitaifa na ushirikishwaji katika uteuzi wa umma; na uwajibishaji wa kutosha.
Mazungumzo hayo yatachukua muda wa siku 60 huku pande hizo zikitarajiwa kutoa maafikiano yao na kutoa mwongozo kwa taifa ya Kenya.