Wasifu wa baadhi ya nyota wanaowania tuzo ya wanariadha bora wa mwaka

Wasifu wa baadhi ya nyota wanaowania tuzo ya wanariadha bora wa mwaka

Wanariadha bora wawili kutoka kila kipengele wanawania tuzo hiyo.
Baadjhi ya wanariadha wanaowania tuzo hiyo./Picha: Getty

Tuzo za wanariadha bora barani Afrika zinatarajiwa kutolewa Disemba mwaka huu, huku majina ya wanariadha wanaotamba kwenye mchezo huo yakitawala vipengele tofauti.

Orodha ya wanariadha wanaowania tuzo hiyo inahusisha wale waliopigiwa kura na Baraza la Riadha ulimwenguni kupitia mitandao ya kijamii.

Wasifu wa Mwanariadha

Letsile Tebogo (Botswana)

Akiwa na umri wa miaka 21, Tebogo anawania tuzo ya mwanariadha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume baada ya kutwaa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki iliyofanyika jijini Paris.

Tebogo alishinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki./Picha: World Athletics 

Tebogo alishinda medali yake ya kwanza ya dhahabu kwa nchi yake.

Alikuwa sehemu ya timu ya Botswana iliyoshinda medali ya fedha kwenye mbio za kupokezana vijiti za mita 400.

Ruth Chepngetich (Kenya)

Mwanariadha huyo anawania nafasi kwa upande wa wanawake.

Alivunja rekodi mbalimbali kutokana na umahiri wake katika mbio.

Mwanariadha wa Kenya Ruth Chepngetich./Picha: World Athletics 

Alikuwa mwanariadha wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuvunja rekodi ya 2:10 katika mbio za marathon zilizofanyika Chicago nchini Marekani.

Tamirat Tola (Ethiopia)

Mfukuza upepo huyo kutoka Ethiopia alishinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki.

Mwanariadha Tamirat Tola kutoka Ethiopia./Picha: World Athletics 

Baadhi ya wanaowania tuzo hiyo

Baadhi ya wanariadha wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na Julien Alfred (Saint Lucia) ambaye alishinda Olimpiki katika mita 100, Sydney McLaughlin-Levrone wa Marekani (Bingwa wa Olimpiki katika kuruka viunzi mita 400), Jakob Ingebrigtsen wa Norway aliyeshinda mita 5000 na Letsile Tebogo wa Botswana aliyeshinda mita 200.

TRT Afrika