Mazinga Ombwe Afrika | Photo: Reuters

na Charles Mgbolu

Ni vijana wa Kiafrika, wengi wao wakiwa katika miaka ya ishirini na tano na kuendelea, wakifanya mazoezi ya sanaa ya kile ambacho mhusika Michael Caine katika filamu ya The Prestige anaelezea kama "kuchukua kitu cha kawaida na kukifanya kitu kisicho cha kawaida". Wakiwa wamesimama mbele ya hadhira inayotazama kwa makini, wakiwa wamedhamiria kukamata kitendo hicho, wanavuta ustadi wao na kuchezesha mikono yanayopumbaza umati na kiinimacho, na kuibua miguno, mayowe na makofi ya kuziba makubwa yenye sauti kubwa.

Mazinga ombwe yako kote barani huku kundi hili la vijana wa Kiafrika ikibuni aina mpya ya burudani, na kujenga hadhira ili iweze kuimarika.

Katika ulimwengu wa magharibi, kuna wana mazinga ombwe maarufu kama vile Dynamo, David Copperfield, Paul Daniels na David Blaine wanashikilia sana mitandao ya kijamii. Wataalamu vijana wa Kiafrika sasa wanaliweka bara hilo kwenye soko, wakiendesha mitindo ya kisasa na kuonesha uwezo wa mitandao ya kijamii kuunda na kuonyesha kiinimacho unaoweza kulinganishwa na wenzetu wa magharibi.

Hawa ni vijana watano ambao TRT Afrika wametambua wanawapa sifa Afrika katika sanaa hio kwa sasa

Babs Cardini (Nigeria)

Babatunde Kasumu Tinubu, almaarufu Babs Cardini, kutoka Lagos ana umri wa miaka 23, na tayari ndiye mwana mazinga ombwe anayejulikana zaidi kutoka Nigeria katika vyombo vya habari vya ndani na kimataifa. "Siku zote nilitaka kuwa Mwana mazinga ombwe. Nilijua huu ulikuwa wito wangu tangu umri wa miaka mitano. Mashabiki wangu wananijua kama mfanya mazingaombwe wa mtaani na kiinimacho," anasema.

Akiwa na zaidi ya wafuasi 300,000 kwenye Instagram, Babs ameunda ulimwengu ya wafuasi wa mazingaombwe. Amefanya maonesho mbele ya watu mashuhuri wa muziki na hata mubashara kwenye runinga, karibu kila wakati akiwaacha watazamaji wake modomo wazi.

Katika video ya mtandaoni inayowashirikisha waimbaji wa Nigeria Davido na Mayorkun, Babs anaonekana akifanya mazinga ombwe ambapo Davido anahisi kuguswa begani mwake, wakati Babs alikuwa akimgusa Mayorkun mahali hapo. Iliwaacha nyota wote wa muziki wakipiga kelele kwa mshangao.

"Kiini macho kina uwezo wa kuleta mwanga furaha ambao huinua kila hali. Huu ndiyo mchango ninayotaka kuleta. Hii ndiyo zawadi ninayotaka kumpa kila mtu, haswa vijana wa Kiafrika ambao wanapitia mengi sasa, "anasema Babs, ambaye aliingia kwenye umaarufu baada ya kumaliza kwa mchujo wa nusu fainali katika kusaka vipaji vya kitaifa huko Lagos.

Mwesigwa Jonathan (Uganda)

Mazinga ombwe yalimfikia Mwesigwa Jonathan akiwa na umri wa miaka 16. Akisema Mmarekani Criss Angel akiwa mtu wa mfano kwake, kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa ameweza kuboresha ufundi wake na kuwa mmoja wa wana mazingw ombwe wazuri zaidi wa Uganda.

“Nilimtazama Criss Angel akifanya mazinga ombwe kwenye TV na nilitaka kumwiga. Kuwa mfanya mazinga ombwe kwangu ilikuwa jambo linalo karibia hali yakuwa shujaa kama wale kwenye filamu. Nilitaka kuwa mtu ambaye angekuwa mfano kwa vijana, kama shujaa mkuu," Jonathan anaiambia TRT Afrika.

Mazinga ombwe Uganda bado lina soko ndogo, ila Jonathan tayari anaogelea na samaki wakubwa, kutumbuiza kwenye tafrija za mashirika ya kimataifa na kutizamwa katika vyombo vya habari vya Uganda.

"Bado sijawa mkubwa sana kwenye mitandao ya kijamii, lakini naanza kupata usikivu. Vijana wengi wanaona video zangu na kunitumia DM, wakisema jinsi wanavyohamasishwa na uvumilivu wangu licha ya vikwazo vyote hapa Uganda. Watu waliofanya mazinga ombwe mitaani siku za nyuma hapa waliwakilisha vibaya ufundi huo. Waliichafua sanaa na kuifanya kiini macho kuonekana kama giza na uovu, ambayo sivyo," anaeleza.

"Hii imeathiri jinsi watu wanavyowaona na namna wanavyowachukulia hapa, na ninajaribu kwa bidii kurekebisha dhana hiyo. Haikuwa rahisi, lakini nimedhamiria kufanya kazi kwa bidii katika ufundi wangu na kubadilisha simulizi hii."

Jonathan ana ndoto ya kufika kwenye daraja ya heshima la Mazinga ombwe. "Nataka siku moja nifanye shoo Las Vegas. Hapo ndio makao makuu ya kiini macho. Hiyo itakuwa siku ambayo ndoto yangu kubwa itatimia," asema.

Bernard Badu Arkoh (Ghana)

Tofauti na Jonathan, Bernard Badu Arkoh, mwenye miaka 27, anayejulikana kwa mashibiki wake kama Mzinga Ombwe Bernard, hakuenda mbali kupata hamasa. Aliipata nyumbani.

“Baba yangu alikuwa mfanya mazinga ombwe. Niliingia kwenye viatu vyake kwa sababu sikutaka kumsahau ... kwa sababu mara kwa mara nahamasishwa na yeye. Ninataka kumfanya ajivunie kila mara," Bernard anaiambia TRT Afrika.

Mhandisi wa umeme kwa mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah, Bernard alihitimu mwaka wa 2018 na kufundisha kama msaidizi wa kufundisha katika alma mater yake kabla ya kazi mbadala ya sanaa ya kiinimacho kuanza.

Mkufunzi huyo wa SAT, GRE na Math Olympiad aliye na tajriba ya zaidi ya miaka 8 alianza kufanya mazinga ombwe kitaaluma mwaka 2018. Kabla ya hapo, alikuwa ametumbuiza katika shule ya sekondari pekee yake.

Bernard hajafanya vibaya tangu wakati huo, baada ya kuwavutia watazamaji wa nchini Ghana pamoja na viongozi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais wa Ghana. "Nataka kuonyesha uwezo wangu kwenye Kombe la Dunia. Hiyo ndiyo ndoto yangu kubwa," anasema mfanya mazinga ombwe huyo mchanga, ambaye mifano yake mingine ni David Copperfield, David Blaine na JS Magic.

Kelvin Kimotho (Kenya)

Kelvin Kimotho, almaarufu Kay the Magician, ndiye mshindi wa hivi karibuni wa onyesho la kusaka vipaji la Talanta Mtaani nchini Kenya. Amekuwa akifanya mazinga ombwe kwa miaka 13, shauku ambayo anahisi imekuwa matibabu kwake kwa njia zaidi ya moja.

"Nilipenda mazinga ombwe baada ya kuona David Blaine maarufu akitumbuiza kwenye TV," kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 aliiambia TRT Afrika.

Akiwa mtoto, Kelvin aligundulika kuwa na ugonjwa wa kukosa umakini/ushupavu kupita kiasi (ADHD), hali ambayo inaweza kuwafanya watoto washindwe kuwa makini, kudhibiti tabia za msukumo au kuwa na shughuli nyingi kupita kiasi.

"Kuwa mwana mazinga ombwe kumesaidia kukabiliana na dalili zangu nyingi," anasema. "Nilielekeza nguvu kutoka kwa shughuli yangu kubwa hadi kuwa mwenye kufikiria sana, kudhibitiwa, na mbunifu. Hili lilinisaidia sana nilipoanza kufanya hila za mazinga ombwe."

Kelvin sasa anajulikana sana nchini Kenya na kwingineko kama mfanya mazinga ombwe na kipaji maalum cha mbinu za kadi.

Anotidaishe Chikaka (Zimbabwe)

Ana umri wa miaka 23 na amekuwa akifanya mazinga ombwe wa kustaajabisha kwa watazamaji waliochanganyikiwa nchini kwao Zimbabwe kwa miaka mitano. Anotidaishe Chikaka, almaarufu Vortex, pia ni msanii wa hip hop na aliteuliwa kwa kipengele cha Best Supporting Hip Hop Act mwaka jana katika Tuzo za kila mwaka za Changamire Hip Hop, mojawapo ya tamasha maarufu zaidi ya muziki nchini Zimbabwe.

Vortex anajulikana kwa maonyesho yake ya mitaani ya moja kwa moja, ambayo video zake zimeenea kwenye mitandao ya kijamii ya Zimbabwe mara kadhaa. "Ninafanya hivi kwa sababu ninataka kuwafanya watu watabasamu na kuwa na furaha. Sifanyi hivi kwa ajili ya umaarufu," anaiambia TRT Afrika.

Kama wafanya mazinga ombwe wote chipukizi, Vortex hupata msukumo kutoka kwa waliobobea zaidi katika hii biashara. Anavutiwa na kazi ya Shin Lim na Spidey, mtaalamu wa mtu apumbazaye akili anayejulikana kwa utaratibu wake wa kutumia kadi.

“Mazinga ombwe bado ni changa nchini Zimbabwe, lakini nafurahi kuwa sehemu ya jitihada za kuipa mwelekeo na kusaidia kuhamasisha kizazi kipya kinachopenda sanaa na kutaka kuwa sehemu yake,” anasema.

TRT Afrika na mashirika ya habari