Saba kati ya wachezaji 10 wa timu ya taifa ya mpira wa handiboli wa Burundi kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19, wanashikiliwa nchini Ubelgiji.
Wachezaji hao wamewekwa kizuizini baada ya kupatikana nchini Ubelgiji na mamlaka ya uhamiaji tangu walipotoweka nchini Croatia mwezi Agosti mwaka huu.
Saba hao ni kati ya wachezaji 10 wa timu ya taifa ya mpira wa handiboli wa Burundi walioomba hifadhi Ubelgiji, ingawa wawili kati yao tayari wameamrishwa waondoke nchini humo.
Licha ya Ubelgiji, kuwa wakoloni wa zamani wa Burundi, na kushuhudia idadi kubwa ya raia wa Burundi, imechukua hatua ya kuwaweka katika kituo kilichofungwa wiki iliyopita, ikisema kuwa wamezidi umri ya kupokewa kama watoto.
Akithibitisha kuzuiliwa kwa wachezaji hao, Waziri wa uhamiaji wa Ubelgiji Nicole de Moor, amefafanua kuwa chini ya sheria ya EU, kwa kuwa wachezaji hao sio watoto, ni lazima warudi Croatia, nchi yao ya kwanza ya kuwasili na kuingia Ulaya.
Ofisi ya Uhamiaji ya Ubelgiji iliwafanyia uchunguzi wa umri kwa vipimo vya mifupa kwa makini baada ya kutilia shaka madai yao kuwa wana umri mdogo.
Matokeo ya uchunguzi huo yalisababisha wengi wa wachezaji hao kugunduliwa kuwa watu wazima, na hivyo kuwaweka chini ya vituo vya kuwazuilia raia wa kigeni.
Wachezaji wao walitoweka kutoka kikosi cha Burundi kilichoshiriki Kombe la Dunia la handiboli la U19 (Agosti) huko Croatia.
Kukwepa kwao kulilazimu michuano miwili ya Burundi katika Kombe hilo, iliyoratibiwa kucheza dhidi ya Bahrain na New Zealand tarehe 10 na 11 Agosti kufutwa kwani Burundi haikuwa na wachezaji wa kutosha kuiwakilisha.
Hata hivyo, mashirika ya kuwatetea wahamiaji yameeneo ya kuwashikilia wahamiaji, na kutoa wito kwa serikali ya Ubelgiji kushughulikia maombi ya wachezaji hao ya kutaka hifadhi.
Kuwarudisha Croatia kungehatarisha maisha yao, mashirika hayo yamesema.