Mkutano huo wa Tabia Nchi wa EAC ni mojawapo ya juhudi za jumuiya hiyo za kuimarisha juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uthabiti wa mabadiliko ya yake, ili kupunguza athari zilizopo, kukuza usalama wa chakula uendelevu na wa mazingira.
Marais na wakuu wa nchi wakiongozwa na mwenyekiti, wa Jumuiya ya EAC, na rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, rais Suluhu Samia wa Tanzania, Rais William Ruto wa Kenya, na Waziri Mkuu wa Rwanda Edouard Ngirente ni miongoni mwa wakuu walioshiriki kwenye mkutano huo ulioanza Arusha nchini Tanzania.
"Lazima tuwe katika mstari wa mbele kwenye uundaji wa suluhisho za kimkakati kushughulikia athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi na usalama wa chakula katika ukanda wetu wote," mwenyekiti wa mkutano wa wakuu wa nchi za Eac ambaye pia ni Rais wa Burundi na rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye alisema.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewakilishwa kwenye mkutano huo na Rebecca Kadaga ambaye ni naibu Waziri mkuu wa Uganda, na Waziri wa masuala ya Jumuiya ya EAC.
"Rwanda imejitolea kutumia kilimo kinachostahimili hali ya hewa na kusaidia mkoa katika kushughulikia athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi na usalama wa chakula," Waziri mkuu wa Rwanda, Edouard Ngirente amesema.
Kwa upande wake, rais Samia Suluhu wa Tanzania, ametoa wito kwa jumuiya hiyo, kuweka mifumo yake yenyewe na kutenga fedha maalum ili kuboresha mazingira ya eneo lake, “Wana Afrika Mashariki, tunapotegemea misaada kutoka nje, tunachelewa kutekeleza mipango yetu. Tuweke mifumo yetu wenyewe na fedha kwa ajili ya kuboresha mazingira yetu," alisema.
Aidha, rais wa Kenya William Ruto, ameongeza, "Uendelevu wa mazingira ni suala muhimu kwa mkoa wetu. Kenya ikielekea mkutano wa kimataifa wa tabia nchi COP28, tutajaribu kusaini mkataba mpya ambao utasaidia ukuaji unao hali ya hewa."
Mkutano huo pia ulichangiwa na Rebecca Kadaga, Naibu waziri mkuu wa Uganda na Waziri wa Masuala ya EAC, pamoja na wawakilishi wengine kutoka Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliogusia ukuzaji wa tabia nchi, usalama wa chakula na ustahimilivu wa mazingira.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud pia anahudhuria mkutano huo.