Ripoti mpya ya Afrobarometer inaonesha kuwa ujuzi kuhusu mabadiliko ya tabianchi ni mdogo nchini | Picha: Reuters

Ni asilimia 32 tu ya Watanzania wanasema wamesikia kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi, huku kukiwa na uelewa zaidi kwa wakazi wa mijini (46%), ripoti ya utafiti mpya kutoka Ripoti ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini, REPOA, yasema.

Serikali leo imeripoti kuwa na mpango wa kukabiliana na pengo hili la maarifa hata hivyo, kupitia maongezi na Mkurugenzi wa Mazingira TRT Afrika ilipata nafasi yakujua zaidi juu ya mpango wa serikali.

"Aidha hivi sasa Serikali imezindua Mpango Kabambe wa Hifadhi ya Mazingira ambao pamoja na mambo mengine umeainisha maeneo yenye athari kubwa za Mabadiliko ya Tabianchi na imeanisha mikakati ambayo inapaswa kutumiwa na jamii katika kuhumili athari za mabadiliko ya tabianchi." Asema Dkt Andrew M Komba, Mkurugenzi wa Mazingira , Ofisi ya Makamu wa Rais, Tanzania

Serikali imetangaza kuwa ina mpango rasmi wa kutoa elimu ya Mabadiliko ya Tabianchi. Mkakati wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi wa Mwaka 2021 umeainisha wadau mbalimbali watakaohusika, hususani Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa mdau muhimu wa kutoa Elimu husika.

"Kila mwaka Ofisi ya Makamu wa Rais hukutana na Maafisa Mazingira wote ikiwemo waliopo mikoani na katika halmashauri na kutoa mafunzo kuhusu masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi." ameongeza Dkt Komba.

Ripoti hiyo ilifichua nini zaidi?

REPOA ni shirika mwenza upande wa Tanzania wa mtandao wa Utafiti wa Afrobarometer.

Uelewa huu wa wananchi kuhusu hali ya hewa unasimama kama 39% kwa ujumla wakati miongoni mwa wakazi wa vijijini, ufahamu unashuka hadi 24% kati ya wanaume na 25% kati ya wanawake alisema.

Uelewa wa mabadiliko ya hali ya hewa unaongezeka kwa kasi na kiwango cha elimu kwa washiriki, kuanzia 12% tu kwa wale wasio na shule rasmi hadi 72% kwa wale walio na sifa za baada ya sekondari.

Miongoni mwa wananchi wanaofahamu mabadiliko ya tabianchi, 8 kati ya 10 wanasema yanafanya maisha kuwa magumu zaidi huku 31% wakidhani kuwa ni mbaya zaidi na 51% ya kundi hili wanaona kuwa ni mbaya zaidi ripoti inaeleza.

Miongoni mwa wale ambao wamesikia kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, wananchi wengi wanasema serikali inafanya kazi nzuri ya kujaribu kuzuia. Lakini wanaona kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa kama jukumu la pamoja, na wanataka ushirikishwaji mkubwa juu ya suala hilo na wafanyabiashara na viwanda, mataifa yaliyoendelea, na raia wa kawaida pamoja na serikali.

Ripoti hiyo pia inaeleza kupitia ukurasa wao wa Twitter kwamba “Wakati Watanzania wanapeana jukumu la msingi kwa raia wa kawaida katika kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuweka jamii safi, wengi wanasema serikali inapaswa kudhibiti sekta ya uchimbaji wa maliasili kwa uthabiti zaidi ili kulinda mazingira.”

Wananchi wanane kati ya 10 walikuwa na msimamo kwamba serikali inapaswa kudhibiti tasnia ya uchimbaji wa maliasili kwa uthabiti zaidi ili kupunguza athari zake kwa mazingira.

Jambo ambalo pengine ni muhimu zaidi, hata hivyo, ni athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika maisha ya watu huku wananchi wengi wakiripoti baadhi ya mabadiliko ya misimu ya ndani na mifumo ya hali ya hewa, kupungua kwa uzalishaji na uhaba wa chakula katika kipindi cha miaka 5 hadi 10 iliyopita.

"Katika mwaka huu kuanzia 1 April hadi Oktoba 2023 Ofisi itakuwa na wataalamu watatu watakaoishiriki katika mbio za mwenge zitakazofika maeneo yote nchini. Ujumbe Mkuu utakuwa ni namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi." amalizia kueleza Dkt Andrew M Komba, Mkurugenzi wa Mazingira , Ofisi ya Makamu wa Rais, Tanzania katika maongezi yake na TRT Afrika.

Hali kama hiyo ilionekana pia nchini Uganda. Ripoti ya shirika la kiraia la Twaweza, mwishoni mwa mwaka jana, iliripoti kupitia utafiti wao kuwa wananchi walipendekeza njia za kupunguza madhara hayo, ikiwa ni pamoja na juhudi za pamoja kati ya serikali na wananchi, kupanda miti na kufanya kilimo mchanganyiko.

TRT Afrika