Na Charles Mgbolu
Wataalamu wa filamu za kiafrika wanajiandaa kusherehekea kazi bora zilizotolewa mwaka uliopita wakati Tuzo za Uchaguzi wa Watazamaji wa Africa Magic 2024 (AMVCA) zimepangwa kufanyika wikendi hii.
Kuna washindani wazuri kwa kila tuzo katika kila kipengele, na mashabiki watalazimika kusubiri hadi Jumamosi, Mei 11, hatimaye kujua washindi.
Mtengenezaji filamu kutoka Nigeria Bose Oshin ndio ameteuliwa kupata tuzo nyingi zaidi kuliko wote na filamu yake 'Over the Bridge', ikiwa na tuzo 12, zikiwemo Muigizaji Bora wa Kuunga mkono, Muigizaji Bora wa Kike, Muigizaji Bora wa Kike wa Kiongozi, Uendeshaji wa Kamera Bora, na Uhariri Bora.
Hii ilifuatiwa na filamu ya kusisimua ya nyeusi na nyeupe yani Black and White ya 'Mami Wata', iliyoandikwa na kuongozwa na C.J. "Fiery" Obasi, wanaoteuliwa kushinda tuzo 11.
'Breath of Life' na 'Jagun Jagun', pia kutoka Nigeria, kila moja na nafasi ya kushinda tuzo 10.
'A Tribe Called Judah' ya Funke Akindele, ambayo ilikusanya rekodi ya Naira bilioni 1.4 ($996,831), na kuwa filamu ya kwanza ya Nollywood kupata zaidi ya Naira bilioni 1 kwenye sinema, pia ina nafasi ya kushinda kwa Muigizaji Bora wa Kike, Muigizaji Bora wa Msaidizi, na Filamu Bora ya Afrika Magharibi.
Huko Afrika Mashariki, 'Where the River Divides', iliyotayarishwa na mtayarishaji wa filamu kutoka Kenya Matrid Nyagah, na 'Ormoilaa Ogol' (The Strong One), iliyotayarishwa na Evelyn Siololo, zinashindania Filamu Bora ya Asili (Afrika Mashariki).
Wengine katika kipengele hiki ni Wandongwa, iliyotayarishwa na John Kokolo; Nakupenda, iliyotayarishwa na Mwendeshaji wa filamu Tanzania Juma Saada; na Itifaki, iliyoongozwa na Omar Hamza.
Kipengele za majukumu ya kuongoza na kuunga mkono zitakuwa za kufuatiliwa kwa makini mwaka huu kufuatia mabadiliko makubwa yaliyotangazwa na waandaaji mwezi Aprili.
Africa Magic ilisema kwamba vipengele hivi havitaamuliwa tena na raia.
Washindi sasa wataamuliwa na jopo maalum la majaji, likiongozwa kwa mara ya nane na mtengenezaji filamu mkongwe na msomi wa vyombo vya habari Femi Odugbemi - ambaye pia ni mwanachama wa Tuzo za Academy of Motion Picture Arts and Sciences (The Oscars) nchini Marekani.
"Kwa tunavyoadhimisha maadhimisho ya miaka kumi, tunaingia katika safari thabiti ya kutathmini upya vipengele vyetu vya tuzo na kuendana zaidi na mwelekeo wa kimataifa na viwango," Mkuu wa Maudhui na Vituo Afrika Magharibi, MultiChoice, Busola Tejumola, alitangaza katika ujumbe wa video.
Mwaka jana, AMVCA ilikosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii baada ya washindi wa baadhi ya vipengele kutangazwa.
Wakosoaji walisema tuzo za Muigizaji Bora wa Kiume/Muigizaji Bora wa Kike hazipaswi kuamuliwa kwa kura za umma, kwani waigizaji maarufu wenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii huishia kuwa washindi na sio muigizaji mwenye ujuzi bora wa uigizaji.