Mama mzazi wa mwimbaji wa Tanzania na msanii maarufu Afrika, Diamond Platnumz, Sanura Kassim anayejulikana 'Mama Dangote' amewashauri wasanii wanaoibuka kujiepusha na tabia zinazoathiri safari yao kwenye sanaa.
"Nilijua kipaji cha mwanangu (Diamond Platnumz) akiwa na miaka 2. Sikukikalia kipaji chake wala sikukificha. Nilimuendeleza na nikawa naye bega kwa bega mpaka leo amekuwa tegemezi letu."
Akizungumza katika mahojiano yake ya kueleza safari ya mwanawe na ushauri wake kwenye sanaa kufuatia ufanisi wa mwanawe, mama Dangote, amewataka wasanii kutokuwa na dharau.
"Msanii yeyote, akiingia lebo yeyote, analeta madharau akishapata umaarufu," alisema.
Msanii akijiunga na nembo yoyote, awe na akili yake, ajue kuwa anaenda kufanya kazi. Ajiepushe na usupastaa. Usupastaa unaponza," alisema.
Aidha, mama Platnumz ameongeza kuwa mwanawe amesalia kuwa motisha kwa watoto wengi wenye vipaji kwani amejitahidi toka udogoni, akimuahidi kuwa atapambana.
Mama Dangote ametoa wasia wake kwa wazazi, wasilalie vipaji vya watoto wao na kuwapa motisha wakiwa wangali wadogo.
"Nilijua kipaji cha mwanangu (Diamond Platnumz) akiwa na miaka 2. Sikukikalia kipaji chake wala sikukificha. Nilimuendeleza na nikawa naye bega kwa bega mpaka leo amekuwa tegemezi letu.
"Ninachowashauri wazazi, ukimwona mwanao ana kipaji, msukume ili akiendeleze kipaji hicho. Asimfungie, asimfiche." mama Dangote anasimulia.
Mama huyo amemtetea mwanae kwa kusema, kuwa mchango wake kwenye sekta ya muziki Tanzania, imeleta ufanisi sio tu katika sanaa bali kwa familia nyengine kwani, kila kipaji alichokiinua, Mungu amekuwa akimpa mwanae pia mafanikio makubwa.