Kwa ujumla, mashabiki hushangaa wanapogundua majina halisi ya wasanii maarufu kwani wasanii hao hujulikana tu kwa majina ya 'usanii' waliyofupisha au kujipa.
Rapa maarufu Tanzania Prof. Jay alipochaguliwa mbunge wa Mikumi, mkoani Morogoro jina lake rasmi, Joseph Haule ndilo lilianza kutumika zaidi bungeni na katika kazi zake zote rasmi.
Wasanii na wahusika wa sanaa nao walifuata nyayo hizo huku, Babu Tale, naye akigeuka kutumia majina yake rasmi Hamisi Shaban Taletale akiwa mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki. Aidha Mwana FA, Mbunge wa Muheza, majina kamili Hamis Mohamed Mwinjuma ni msanii mwingine ambaye ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania.
Omari Faraji Nyembo - Ommy Dimpoz
Mwimbaji wa Uganda Jose Chameleone ndiye Joseph Mayanja
Otile Brown anajulikana kwa majina rasmi Jacob Obunga
Raymond Shaban Mwakyusa ndiye Rayvanny
Haya basi Mbosso Khan ndiye anajulikana Mbwana Yusuf Kilungi kwenye vyeti vyake na stakabadhi rasmi.
Kigogo Jay Melody naye anaitwa majina rasmi Sharifu Said Juma
Msanii Mr. Love byte, Lava Lava anafahamika kama Abdul Juma Idd
Konde Boy, Harmonize, anaitwa Rajab Abdul Kahali na ndio majina yake halisi.
Rapa wa Kenya Khaligraph Jones ambaye hivi karibuni aliuwasha moto na kuzua mjadala wa ubabe wa rap kati ya Kenya na Tanzania, ndiye Brian Ouko Omollo
Msanii maarufu wa Tanzania Roma, ndiye Ibrahimu Mussa huku rapa mwingine Nay wa Mitego naye akiitwa Emmanuel Elibariki
Hata hivyo, kwa mwimbaji Aslay, jina la Aslay pia ndilo jina lake rasmi huku majina yake kamili yakiwa Aslay Isihaka Nassoro.
Msanii mwingine, Rosa Ree, naye anaitwa Rosary Robert Iwole huku malkia mwingine wa Bongo Fleva Nandy, akijulikana kama Faustina Charles Mfinanga.
Orodha ni ndefu lakini hata hivyo, majina yote huwa muhimu kwani moja ni la kusaka unga huku jengine likiwa ndio linalotumika rasmi kutimiza masharti haswa wakati wa kusafiri, kusaini mikataba na hata kupokea huduma muhimu ndani na nje ya nchi.