Mwimbaji Diamond Platnumz ndiye anayeongoza Instagram Tanzania/ Picha: Diamond Platnumz

Mtandao wa Instagram unajitofautisha kama jukwaa linalopendelewa sana Tanzania na lenye ushawishi, ikijivunia mabilioni ya watumiaji kote duniani wanaofanya. Katika taarifa hii, tunazungumzia juu ya akaunti zinazofuatwa zaidi za Instagram Tanzania.

Mwanamuziki Diamond Platnumz ndiye mtu anayefuatwa zaidi Kwenye Instagram Tanzania kwani na zaidi ya wafuasi 16.6 milioni.

Millard Ayo ambaye ni mwandishi maarufu na mshindi wa Tuzo za utangazaji kwenye TV na Redio ndiye wa pili akiwa na wafuasi 13.3 milioni.

Aidha, Wema Sepetu anakaribia wafuasi milioni 11 kwani mpaka sasa ana wafuasi 10.9 milioni kwenye Instagram.

Hamissa Mobetto, mwimbaji na mwanamitindo, ana wafuasi milioni 10.6 na ni baadhi ya watu maarufu katika sekta ya sanaa Tanzania mwenye zaidi ya wafuasi milioni 10.

Harmonize milioni 9.7, Ray Vanny milioni 9.5, Ali Kiba milioni 9.3, na Nandy milioni 9, ndio wanaongoza orodha ya watu maarufu wenye wafuasi zaidi ya milioni 9.

Kwenye orodha ya watu wenye wafuasi kati ya milioni 8 na milioni 6 ni muimbaji na muigizaji, Vanessa Mdee mwenye wafuasi milioni 8.6 akifuatwa na Idris Sultan ambaye ni mwigizaji maarufu, na mchekeshaji mwenye milioni 8.5, na Mange Kimambi mwenye milioni 7.4.

Kwenye orodha ya watu wenye wafuasi kati ya milioni 8 na milioni 6 ni mwimbaji Vanessa Mdee mwenye wafuasi milioni 8.6 akifuatwa na Idris Sultan ambaye ni mwigizaji maarufu, na mchekeshaji mwenye wafuasi milioni 8.5, na Mange Kimambi mwenye wafuasi milioni 7.4.

TRT Afrika