Picha ya Benki ya Tanzania, Dar es Salaam / Picha: Reuters

Kiwango hiki kipya ni cha chini sana ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, eneo ambalo uchumi wake unakabiliwa na changamoto za kupanda kwa bei zinazosababishwa na kutokuwa imara kwa bei za bidhaa za kimataifa, vita vya Ukraine, ukame na migogoro ya kisiasa katika baadhi ya nchi, pamoja na sababu nyingine.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilisema kupungua huko kulitokana kwa kiasi kikubwa na "kupungua kwa bei za chakula na bidhaa zisizo za chakula, kufuatana na kupungua kwa bei ya bidhaa za watumiaji katika soko la kimataifa."

Kiwango rasmi cha mfumuko wa bei nchini Uganda kilikuwa asilimia 4.9, Kenya ilikuwa asilimia 7.9, Rwanda ilikuwa asilimia 20.4, wakati kiwango cha Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kilikuwa asilimia 28.9 na 26.67 mtawalia mwezi wa Mei. Kiwango cha rasmi cha Sudan Kusini kilikuwa asilimia 5.6 mwezi wa Juni.

TRT Afrika