Serikali ya Uganda inatabiri uchumi wake utaongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka wa fedha wa 2023/24 utakaomalizika mwezi Juni 2024.
Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, hilo litakuwa ongezeko litakalochangiwa na ukuaji unaotarajiwa mwaka huu kupitia sekta za viwanda, huduma na kilimo.
Waziri wa Fedha Matia Kasaija amesema deni la taifa ambalo ni asilimia ya pato la taifa (GDP) limepungua kutoka 48.4% mwaka mmoja uliopita hadi kufikia asilimia 47 mwishoni mwa Juni mwaka huu.
Kulikuwa na "ongezeko dogo la mkusanyiko wa madeni, sambamba na ahadi za serikali za kuimarisha fedha," Kasaija alisema kwenye hafla ambayo aliwasilisha mkakati wa bajeti ya serikali.
Kwa jumla, deni la taifa kufikia mwishoni mwa Juni lilikuwa shilingi trilioni 86.8 za Uganda (dola billion 23.33i), ikilinganishwa na shilingi trilioni 78.8 mnamo Juni 2022, lakini ukuaji wa uchumi ulimaanisha kuwa sehemu yake ya pato la taifa ilipungua.
Mwezi uliopita, Benki ya Dunia ilisitisha mikopo yote mipya kwa Uganda kupinga kupitishwa kwa sheria mpya ya kupambana na wapenzi wa jinsia moja.
Mwezi huu, Shirika la Ukadiriaji Fitch lilithibitisha ukadiriaji wa Uganda Katika kiwango cha B+ kwa mtazamo hasi, likitaja matatizo ya kupokea mikopo ya bei nafuu baada ya Benki ya Dunia kuichukulia hatua.
Kwa ujumla ukuaji wa uchumi wa Uganda unatarajiwa kufikia dola bilioni 63.36 za Marekani mwaka 2024/25, kulingana na wizara huyo wa fedha, Matia Kasaija.
Kasaija aliongeza kuwa vipaumbele vya ufadhili ndani ya mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kuharakisha ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta, huku serikali ikigharamia wingi wa ufadhili kwa mradi huo badala ya kusaka msaada kutoka kwa wawekezaji binafsi.
Mkataba wa awali na mashirika ya kimataifa unaojumuisha kitengo cha Kampuni ya Marekani ya Baker Hughes BAKERO ili kufadhili kiwanda cha kusafisha mafuta ulivunjika mwezi Julai.
Uganda na makampuni ya kimataifa ya mafuta kama Totalenergies ya Ufaransa TTEF.PA, na Cnooc ya China 0883.HK pia wanatekeleza miradi ya mabilioni ya dola ikiwa ni pamoja na bomba la mafuta ghafi. Uzalishaji wa mafuta ya kibiashara unatarajiwa kuanza mwaka 2025.