Watalii wakishuhudia simba ndani ya hifadhi ya Serengeti./Picha: Getty

Ukanda wa Afrika Mashariki umeshuhudia mafaniko ya sekta ya utalii, kutokana na idadi ya wageni na mapato yanayopatikana kupitia shughuli hiyo.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni, nchi hizo zimeshuhudia ongezeko la watalii wanaotembelea vivutio mbalimbali vinayopatikana katika nchi hizo.

Tanzania, ambayo inasifika kwa kuwa na hifadhi ya taifa ya Serengeti, ambayo ni hifadhi bora zaidi barani Afrika na mlima Kilimanjaro, iliingiza Dola za Kimarekani milioni 3.4, kupitia watalii zaidi ya milioni 1.8 walioitembelea nchi hiyo kwa kipindi cha mwaka jana.

Ukanda wa Afrika Mashariki umeshuhudia mafaniko ya sekta ya utalii, kutokana na idadi ya wageni na mapato yanayopatikana kupitia shughuli hiyo./Picha: Getty

Kulingana Wizara ya Utalii ya nchi hiyo, Kenya ilipokea zaidi ya wageni milioni mbili kwa mwaka 2023, na hivyo kujihakikishia kiasi cha cha zaidi ya dola bilioni 2.7.

Mbali na hifadhi ya Masai Mara, nchi ya Kenya inajulikana kwa idadi nyingi ya wanyamapori wanaopatikana ndani ya hifadhi ya taifa ya Meru.

Tembo akijivinjari ndani ya hifadhi ya taifa ya Meru nchini Kenya./Picha: Getty

Jumla ya watalii milioni 1.4 waliitembelea Rwanda kwa mwaka 2023. Kulingana na Bodi ya Maendeleo ya nchi hiyo, Rwanda ilivuna mapato ya Dola za Kimarekani milioni 620, kutokana kwa sekta ya utalii, kwa kipindi cha 2023.

Kwa upande wake, Uganda ilipata jumla ya Dola za Kimarekani bilioni 1.025 kutokana na wageni milioni 1.2, waliotembelea nchi hiyo mwaka jana.

Takwimu hiyo, ni kwa mujibu wa Wizara ya Utalii ya nchi hiyo.

TRT Afrika